Pata taarifa kuu

India : Mkutano wa G20 waanza wakati baadhi ya viongozi wasusa

Mkutano wa mataifa tajiri na yenye uwezo kiuchumi unaanza rasmi leo Jumamosi Jijini New Delhi nchini India. Kufikia sasa baadhi ya viongozi wameelekea huko akiwemo rais wa marekani Joe Biden wakati huu kukiwa na taarifa kuwa kuna viongozi ambao hawatahudhuria mkutano huo.

Waziri Mkuu Narendra Modi anatarajia kuchukua fursa ya mkutano huu wa G20 ulioandaliwa mjini New Delhi ili kukuza ushawishi wa kidiplomasia wa India unaokua na kuwezesha mazungumzo kuhusu Ukraine au ongezeko la joto duniani bila ya kuwepo kwa Xi Jinping na Vladimir Putin.
Waziri Mkuu Narendra Modi anatarajia kuchukua fursa ya mkutano huu wa G20 ulioandaliwa mjini New Delhi ili kukuza ushawishi wa kidiplomasia wa India unaokua na kuwezesha mazungumzo kuhusu Ukraine au ongezeko la joto duniani bila ya kuwepo kwa Xi Jinping na Vladimir Putin. AP - Manish Swarup
Matangazo ya kibiashara

Hapo siku ya Alhamisi taarifa ya Kremlin ilisema kuwa rais wa Urusi hana nia yashiriki mkutano huo au hata kuhudhuria kwa njia ya vídeo. Rais wa China Xi Jinping pia hatahudhuria mkutano huo.

Rais wa Marekani Joe Biden anatumai kutumia nafasi ya kukosekana kwa viongozi hao wawili , Xi Jinping  na Putin ili kuimarisha ushawishi wa Washington.

Viongozi hao wanakutana wakati huu kukiwa na mgawanyiko mkubwa kufuatia  vita vya Ukraine na jinsi ya kuyasaidia mataifa yanayoinukia kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi. Juzi tuu marekani iliipa msaada wa ndege zisizo na rubani nchi ya Ukraine. Swala ambalo urusi ilisema ni kinyume na ubinaadamu.

Waziri Mkuu wa India Narendra Modi amesisitiza dhamira ya kutanua kundi hilo kwa kujumuisha Umoja wa Afrika kama mwanachama wa kudumu.

Mwaka jana viongozi hao walikutana kwa mkutano wa kilele huko Bali, Indonesia, ili kuleta afueni kwa uchumi unaokumbwa na mgogoro na angalau kuwapatanisha Urusi na Ukraine.

Katika miaka ya hivi karibuni, bara la Afrika limealikwa kwa utaratibu kwenye mikutano ya kilele ya kundi hili. Mwaka huu, uwepo wake ni muhimu zaidi kuliko wakati mwingine wowote kwa kuzingatia majanga mengi yanayoathiri Afrika, iwe uhaba wa chakula, hali ya hewa, nishati au madeni

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.