Pata taarifa kuu

Macron ziarani Bangladesh: Swali la nafasi ya Ufaransa katika Indo-Pasifiki

Baada ya kushiriki katika mkutano wa kilele wa G20 nchini India, rais wa Ufaransa Emmanuel Macron aliwasili Jumapili jioni huko Dhaka, Bangladesh. Ziara ya kwanza ya rais wa Ufaransa katika kipindi cha miaka 33. Ziara hii ni sehemu ya mkakati mpya wa Paris wa Indo-Pasifiki. Ziara ambayo inaambatana na kipengele cha kiuchumi, pamoja na mkataba mkuu wa utoaji wa Airbus kwa shirika la ndege la kitaifa la Biman Bangladesh Airlines.

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron akitia saini kwenye kitabu cha wageni katika makazi ya Baba wa Taifa la Bangladesh, Bangabandhu Sheikh Mujibur Rahman, wakati wa ziara yake huko Dhaka, Jumatatu hii, Septemba 11, 2023.
Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron akitia saini kwenye kitabu cha wageni katika makazi ya Baba wa Taifa la Bangladesh, Bangabandhu Sheikh Mujibur Rahman, wakati wa ziara yake huko Dhaka, Jumatatu hii, Septemba 11, 2023. AFP - LUDOVIC MARIN
Matangazo ya kibiashara

Emmanuel Macron ametangaza kujitolea kwa ndege kumi za Airbus A350. Huu ni mkataba wa kwanza kati ya kampuni ya kutengeneza ndege a Ulaya na Dhaka. Fedha, ambazo kwa sasa zinakamilishwa, zinapaswa kuwa karibu dola bilioni 3.

Kampuni hii imekuwa ikitoa ndege hizo hadi sasa kwa kampuni ya Marekani ya Boeing pekee, anabainisha mwandishi wetu maalum nchini Bangladesh, Dominique Baillard. Kwa hivyo ni tukio la Wazungu na hasa kwa Ufaransa, ambapo kunapatikana viwanda vya Airbus.

Ili kuingia katika mkataba wa kibiashara, inabidi kwanza kutia sahihi makubaliano ya kisiasa. Yote hayo yamefanywa tangu Jumatatu asubuhi. Baada ya kuwasili Jumapili jioni, Emmanuel Macron alipokelewa kwa shangwe na Waziri Mkuu, Sheik Hasina.

Katika suala la anga, barua ya nia pia ilitiwa saini kati ya Airbus Defense na Bangladesh Satellite, kwa ajili ya kuwasilisha satelaiti ya uchunguzi.

Hatimaye, Shiŕika la Maendeleo la Ufaŕansa (AFD) limetia saini mkataba wa ufadhili na seŕikali kwa dola milioni 200 kusaidia maendeleo ya manispaa 86 katika nyanja ya kushughulikia taka, maji ya kunywa au mifereji ya maji ya mvua.

Mwaka wa 2022 uliweka rekodi mpya ya biashara kati ya nchi hizo mbili. Biashara ziliongezeka kwa 50%, kufikia karibu dola bilioni 5.

Uhusiano kati ya Ufaransa na Bangladesh una msingi wa kihistoria. André Malraux, ambaye alikuja huko miaka 50 tu iliyopita, alitoa wito wa uhuru wa nchi hiyo mwaka 1971. Lakini uhusiano huu sasa unahitaji kuanzishwa upya. Ziara ya mwisho ya rais wa Ufaransa ilikuwa katika miaka ya 1990.

Kuwasili kwa Emmanuel Macron ni sehemu ya mkakati mpya wa Ufaransa wa Indo-Pasiifiki. Sambamba na uhusiano na India. Na bila shaka, ziara hii inakuja na sehemu ya kiuchumi. Mbali na ndege, Ufaransa ingependa kuuza vinu vya nyuklia kwa Bangladesh.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.