Pata taarifa kuu

India: Takriban watu 40 wafariki kufuatia mafuriko ya ghafla katika Milima ya Himalaya

Takriban watu 40 wamekufa katika bonde la Himalaya kaskazini mashariki mwa India na maelfu ya wengine wameachwa bila makaazi baada ya mafuriko yaliyosababishwa na kufurika kwa ziwa la barafu Jumatano, kulingana na ripoti mpya kutoka kwa mamlaka leo Ijumaa.

Maji yamesomba kila kitu huko Rangpo, Sikkim, baada ya ziwa kufurika mnamo Oktoba 4, 2023.
Maji yamesomba kila kitu huko Rangpo, Sikkim, baada ya ziwa kufurika mnamo Oktoba 4, 2023. AP - Prakash Adhikari
Matangazo ya kibiashara

"Miili kumi na tisa imepatikana," V.B. Pathak, afisai mkuu wa serikali katika jimbo la Sikkim, ameliambia shirika la habari la AFP.

Katika nchi jirani ya Bengal Magharibi, miili mingine 21 imepatikana katika muda wa siku tatu zilizopita, hakimu wa wilaya hiyo Shama Parveen ameliambia shirika la habari la AFP.

Eneo hili la mbali, lenye milima la Himalaya liko karibu na mpaka wa India na Nepal. Ziwa Lhonak liko chini ya barafu karibu na Kangchenjunga, Mlima watatu mrefu zaidi duniani. 

Idadi ya waliofariki hapo awali iliyotangazwa na mamlaka siku ya Alhamisi ilikuwa angalau 14, lakini timu za utafutaji na uokoaji zilipata miili zaidi usiku wa kuamkia leo Ijumaa maji yakielekea kwenye Ghuba ya Bengal.

Miongoni mwa waliofariki ni wanajeshi sita wa jeshi la India kutoka Sikkim, mji unaopatikana kwenye mpaka wa India na Nepal na China na ambapo kunapatikana idadi kubwa ya wanajeshi.

Takriban watu wengine 8,000 wanapewa hifadhi katika kambi za muda za misaada katika shule, ofisi za serikali na nyumba za wageni, kulingana na taarifa ya serikali ya Sikkim.

Mafuriko na maporomoko ya ardhi hutokea mara kwa mara nchini India na husababisha uharibifu mkubwa, hasa wakati wa msimu wa mvua, ambao huanza mwezi Juni hadi mwezi Septemba. Lakini kufikia mwezi wa Oktoba kipindi hicho kinakuwa kimekwisha.

Wataalamu wanasema mabadiliko ya hali ya hewa yanafanya maafa haya kuwa ya mara kwa mara na makubwa. Kuyeyuka kwa barafu pia huongeza kiwango kikubwa cha maji kwenye mito, wakati ujenzi usiofuata sheria katika maeneo yenye mafuriko pia unaweza kuzidisha uharibifu.

Barafu za Himalaya zinayeyuka kwa kasi zaidi kuliko wakati mwingine wowote kutokana na mabadiliko ya hali ya hewa, na kuwaweka wakazi kwenye majanga yasiyotabirika.

Barafu iliyeyuka kwa kasi ya 65% kati ya 2011 na 2020, ikilinganishwa na miaka kumi iliyopita, kulingana na ripoti iliyotolewa mwezi Juni na Kituo cha Kimataifa cha Maendeleo ya Milima ya Kimataifa.

Kulingana na njia za sasa za utoaji wa gesi chafuzi, barafu zinaweza kupoteza hadi 80% ya ujazo wake wa sasa kufikia mwisho wa karne hii, kulingana na ripoti hiyo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.