Pata taarifa kuu

Blinken nchini India kwa mazungumzo kuhusu China na Israel

Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken atashiriki katika mazungumzo mjini New Delhi siku ya Ijumaa ili kuimarisha ushirikiano na India katika kukabiliana na China kujiimarisha katika eneo la Asia-Pacific, na kupata uungaji wake mkono katika vita kati ya Israel na Hamas.

Rais wa Marekani Joe Biden na Waziri wa Mambo ya Nje Antony Blinken, katika mkutano kwa njia ya video na Waziri Mkuu wa India Narendra Modi, Aprili 11, 2022.
Rais wa Marekani Joe Biden na Waziri wa Mambo ya Nje Antony Blinken, katika mkutano kwa njia ya video na Waziri Mkuu wa India Narendra Modi, Aprili 11, 2022. REUTERS - KEVIN LAMARQUE
Matangazo ya kibiashara

Bw Blinken na Waziri wa Ulinzi wa Marekani Lloyd Austin wanatarajiwa kukutana na Waziri wa Mambo ya Nje wa India Subrahmanyam Jaishankar na Waziri wa Ulinzi Rajnath Singh mjini New Delhi kwa mazungumzo ya kila mwaka ya nchi "mbili + mbili".

Kwa mujibu wa Bw. Jaishankar, mazungumzo hayo yatazingatia "ushirikiano wa ulinzi na usalama."

India, mwanachama wa "Quad", muungano wa ushirikiano wa kiulinzi pamoja na Marekani, Australia na Japan, inajiweka kama ngome dhidi ya matarajio ya China yanayozidi kuwa na msimamo katika eneo hilo la Asia Pacific.

Washington inatumai kuwa uhusiano wa karibu wa ulinzi utasaidia kutenganisha India na Urusi, msambazaji mkuu wa silaha wa New Delhi.

- "Haja ya ulinzi" -

"Nia yetu ni kuhimiza ushirikiano zaidi ili kutengeneza vifaa vya ulinzi vya kiwango cha kimataifa ili kukidhi mahitaji ya ulinzi ya India na kuchangia usalama zaidi wa kimataifa," amesema Donald Lu, mwanadiplomasia mkuu wa Marekani katika ukanda wa  Asia Kusini na Asia ya Kati.

Kutoka Korea Kusini, Bw. Blinken aliwasili katika mji mkuu wa India Alhamisi jioni, hatua ya mwisho ya ziara ya ambayo ilimpeleka Mashariki ya Kati lakini pia Japan ambako alihudhuria mkutano wa mawaziri wa mambo ya Nje wa G7 kutafuta mwafaka baada ya zaidi ya mwezi mmoja wa vita kati ya Israel na Hamas.

India, iliyoharakia kulaani Hamas baada ya mashambulizi ya Israel mnamo Oktoba 7, inashiriki msimamo wa Washington wa kuunga mkono kuundwa kwa taifa huru la Palestina.

"Serikali ya India imekuwa moja kwa moja katika kulaani shambulio la kigaidi la Hamas na pia imejiunga na mataifa mengine, ikiwa ni pamoja na Marekani, ambao wametoa wito wa upatikanaji endelevu wa kibinadamu kwa Gaza," Bw.

Waziri Mkuu Narendra Modi alitangaza "mshikamano wake na Israeli" na India ilituma msaada nchini Misri kwa raia wa Palestina katika Ukanda wa Gaza uliozingirwa.

Mzozo wa sasa unaleta changamoto kubwa kwa mipango ya kuunda njia ya biashara inayounganisha Ulaya, Mashariki ya Kati na India, iliyozinduliwa katika mkutano wa G20 mjini Delhi mwezi Septemba.

"Pamoja na India, tunashiriki malengo ya kuzuia kuenea kwa mzozo huu, kuhifadhi utulivu katika Mashariki ya Kati na kuendeleza suluhisho la serikali mbili," Lu ameongeza.

- "Indo-Pasifiki kuwa huru, wazi, yenye mafanikio na salama -

"Tutavutiwa kujua jinsi yanavyoendelea majadiliano kati ya India na China kuhusu masuala ya mpaka," Bw. Lu pia alionyesha.

Migogoro ya muda mrefu ya mpaka katika Himalaya bado ni chanzo cha mvutano kati ya India na China. Mnamo mwezi Juni 2020, mapigano kati ya wanajeshi wa India na China yaliripotiwa huko Ladakh (kaskazini mwa India).

"Moja ya hoja nyingi za majadiliano itakuwa ushirikiano wetu na India kuweka Indo-Pasifiki huru, wazi, yenye mafanikio na salama," alisema.

Usemi huu wa mwisho ni kwa Washington, njia ya kukosoa kwa namna iliyofichika, China na matarajio yake ya kiuchumi na ya kimaeneo na ya kimkakati katika kanda.

India imelazimika kusawazisha muungano wake wa kitamaduni na Urusi, ambayo imetoa silaha zake nyingi na ununuzi wa mafuta uliopunguzwa bei tangu uvamizi wa Urusi nchini Ukraine, na kuongezeka kwa maelewano na Washington.

Uvamizi wa Urusi kwa Ukraine pia utakuwa kwenye ajenda, Lu amebainisha.

Utawala wa Marekani umetanguliza uhusiano na India, unaoonekana kama mshirika kugawana wasiwasi sawa na China, lakini ugomvi wa hivi karibuni kati ya New Delhi na Ottawa, mshirika wa zamani wa Marekani, unaweza kumwaibisha Bw. Blinken.

Uhusiano kati ya India na Canada ulidorora mnamo mwezi Septemba wakati Waziri Mkuu Justin Trudeau alipohusisha hadharani idara za kijasusi za India katika mauaji ya Mcanada mwenye asili ya India.

Mamlaka ya India, ambayo ilielezea dhana hii kama "upuuzi", ilikuwa ikitafuta ugaidi na njama iliyosababisha mauaji ya  Hardeep Singh Nijjar ambaye alifanya kampeni ya kuundwa kwa jimbo la Sikh, huru kutoka kwa India.

"Tumeitaka serikali ya India kwa uwazi na kwa faragha kushirikiana na Canada katika uchunguzi wa tuhuma hizi," Lu amesema. "Tunatumai kwamba uchunguzi wa Canada utaendelea na kwamba wahusika watafikishwa mahakamani".

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.