Pata taarifa kuu

Tetemeko la ardhi lasababisha maafa nchini China

Watu zaidi ya 100 wameuwa na wengine zaidi ya 200 wamejeruhiwa baada ya kutokea kwa tetemeko la ardhi, Kaskazini Magharibi mwa China. 

Tetemeko la ardhi nchini China
Tetemeko la ardhi nchini China AP - Zhang Hongxiang
Matangazo ya kibiashara

Tetemeko hilo lenye ukubwa wa ritcha 5.9 limetokea katika mkoa wa Gansu, usiku wa manane na kusababisha maafa, pamoja na uharibifu wa majengo.

Kumeripotiwa pia tetemeko la pili katika maeneo ya Xinjiang, Jumanne asubuhi, lakini taarifa za kina hazijafahamika.

Picha na mikanda ya video, inaonesha hospitali zikiwapokea watu walioathiriwa, huku jitihada za kuwatafuta watu wengine waliofunikwa na vifusi zikiendelea.

Umeme pamoja na huduma za maji, zimekatika katika mkoa huo, katika eneo ambalo matetemeko ya ardhi hutokea mara kwa mara. Mwezi Septemba watu wengine 60 waliuawa katika jimbo la Sichuan.

Rais Xi Jinping, ameagiza watalaam wa uokoaji kufanya kila linalowezekana kuwasaidia watu waliothiriwa na tetemeko hilo la ardhi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.