Pata taarifa kuu
Syria

Kofi Annan asema Syria imekubali kutekeleza mapendekezo yake

Mpatanishi wa Mgogoro wa Syria kutoka Umoja wa Mataifa UN na Jumuiya ya Nchi za Kiarabu Kofi Annan ameliambia Baraza la Usalama la Umoja huo kuwa serikali ya Rais Bashar Al Assad imekubali kutekeleza mapendekezo yake sita ifikapo tarehe kumi ya mwezi huu.

REUTERS/Denis Sinyakov
Matangazo ya kibiashara

Annan amekuambia kikao Cha Baraza la Usalama hatua hiyo ni ya kupongezwa na akaomba aendelea kupatiwa ushirikiano katika kuhakikisha mpango wake wa kumaliza umwagaji damu nchini Syria unafanikiwa.

Balozi wa Marekani katika Umoja wa Mataifa UN Susan Rice amepongeza hatua hiyo ya Annan na kutaka kuona utekelezaji wake kutoka kwa serikali ya Syria.

Naye Balozi wa Syria katika Umoja huo Bashar Jaafari amesema wao wapo tayari kuendelea kushirikiana na Anna katika kuhakikisha mgogoro huo unapatiwa ufumbuzi.

Taarifa hizi zinakuja wakati huu ambapo Mkuu wa Shirika la Msalaba Mwekundu Duniani ICRC Jakob Kellenberger akitangaaza kuaza kwa mpango mpya wa kusaidia waathirika hao wa Syria.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.