Pata taarifa kuu
UFILIPINO

Hatimaye misaada yaanza kuwafikia manusura wa kimbunga Haiyan nchini Ufilipino

Hatimaye misaada ya chakula na matibabu leo Jumamosi imeanza kuwafikia waathirika wa kimbunga Hyan waliokuwa wamekata tamaa nchini Ufilipino ingawa makundi ya kibinadamu yameonya kuhusu changamoto kubwa katika kufika maeneo ya kijijini katika kisiwa hicho. 

Taswira ya jimbo la Tacloban nchini Ufilipino
Taswira ya jimbo la Tacloban nchini Ufilipino telegraph.co.uk
Matangazo ya kibiashara

Kimbunga hicho cha aina yake kilichopiga nchini humo mnamo Novemba 8 pamoja na ukubwa wa uharibifu wake, kwa kiasi kikubwa kilitatiza juhudi za uokozi, na kuacha mamilioni ya watu katika hali mbaya ya majeraha, njaa, ukosefu wa makazi, ukosefu wa umeme na maji,hasa kwenye visiwa vya Leyte na Samar.

Mashirika ya Umoja wa Mataifa yamesema kuwa zaidi ya watu 170,000 wamepokea mgawo wa mchele ama pakiti za chakula, wakati madaktari wasio na mipaka na shirika la Msalaba Mwekundu wamesema kuwa watakuwa na vitengo vya upasuaji vinavyotembea na vingine vitafanya kazi kwenye jimbo la Tacloban mwishoni mwa wiki.

Juhudi za misaada ya kibinadamu nchini Ufilipino zimepiga hatua kwa sasa kutokana na msaada unaoongozwa na kundi la wanaanga wa Marekani siku nane baada ya kimbunga kikubwa kiitwacho Haiyan kugharimu maisha ya maelfu ya watu na mamilioni wengine kukosa makazi.

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.