Pata taarifa kuu

Hofu ya mzozo wa kiuchumi yatishia raia Ukraine

Wakati mataifa makubwa na taasisi za kimataifa zikijaribu kukutana kuisaidia Ukraine raia wa kawaida wa Ukraine wameingiwa na hofu ya kutopata kipato.

Raia wa Ukraine wakiandamana kupinga uvamizi wa majeshi ya Urusi huko Crimea
Raia wa Ukraine wakiandamana kupinga uvamizi wa majeshi ya Urusi huko Crimea REUTERS/Mike Theiler
Matangazo ya kibiashara

Wanunuzi wa bidhaa wameonekana wachache katika maeneo mbalimbali nchini Ukraine wakati huu wakihofia tatizo la kiuchumi huenda likaathiri kwa kiwango cha juu hivyo kupunguza matumizi ya fedha zao.

Raia wanasema wanajaribu kujiandaa kwa kuhifadhi pesa zao huenda hali ya mambo ikabadilika na kuwa mbaya zaidi.

Viongozi wa Umoja wa Ulaya wameendelea kuwa na mazungumzo na utawala wa Kiev nchini Ukraine kujaribu kufikia muafaka kuhusu kuendelea kuiwezesha kifedha nchi hiyo ili kukabiliana na mzozo wa kiuchumi ambao huenda ukaikumba nchi hiyo kutokana na mgogoro wa kisiasa unaoshuhudiwa kwasasa.

Ujumbe wa viongozi wa Umoja wa Ulaya walikutana mjini Brussels kwa mazungumzo na waziri mkuu wa Ukraine ambapo kwa pamoja walikubaliana kimsingi kuendelea kuisaidia nchi hiyo kiuchumi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.