Pata taarifa kuu
VENEZUELA-Mazungumzo

Umoja wa Amerika ya Kusini umeanzisha jitihada za kupatikana kwa suluhu kati ya serikali ya Venezuela na upinzani

Kufuatia wiki kadhaa za maandamano ya vurugu, hatimaye Serikali ya venezuela imekubalia waangalizi wa kigeni kuingia nchini humo kujaribu kumaliza mzozo wa kisiasa ulioikumba nchi hiyo. Mgogoro huo sasa utasuluhishwa chini ya usimamizi wa mawaziri wa mambo ya kigeni toka jumuiya ya mataifa ya Amerika Kusini ambao watakuwa na jukumu moja tu, la kuhakikisha suluhu inapatikana kati ya serikali na Upinzani.

Rais wa Venezuela, Nicolas Maduro akikutana kwa mazungumzo na mawaziri wa mamabo ya nje wa Amerika ya kusini.
Rais wa Venezuela, Nicolas Maduro akikutana kwa mazungumzo na mawaziri wa mamabo ya nje wa Amerika ya kusini. Jorge Silva / Reuters
Matangazo ya kibiashara

Toka mwanzoni mwa mwezi February watu wanaokadiriwa kufikia 34 wamepoteza maisha na wengine 500 wamejeruhiwa kutokana na vurugu za maandamano ya upinzani wanopinga utawala wa Maduro na hali ngumu ya maisha nchini humo.

Hata hivi bado kuna milipuko ya mara kwa mara ya vurugu mitaani, huku baadhi ya wafuasi wa upinzani waliyokua wakianadamana wakiwa bado wanaziwiliwa jela kwa madai ya kuchochea vurugu.

Maduro aliitisha mazungumzo hivi karibuni baada ya maandamano kuanza, lakini Kiongozi wa chama kikuu cha upinzani amekataa kushiriki mazungumzo hayo, akisema kuwa wao hawana imani na serikali , wanataka wapatanishi wasimamiye mazungumzo na kudai kutolewa kwa wafuasi wao wanaoziwiliwa jela.

-
Baada ya ziara ya siku mbili nchini Venezuela , mawaziri wa mambo ya kigeni kutoka Umoja wa Amerika ya Kusini ( UNASUR ) wamesema jana kwamba wamekubaliana na rais Maduro wamekubaliana kuwa na nia njema ya kuanzisha mazungumzo ili kutafuta suluhu ya mgogoro unaoendelea nchini Venezuela.

Maduro amesema kwamba ameomba Umoja wa Amerika ya Kusini kuwa angekuwa (UNASUR), kuteua kundi la mawaziri wa mambo ya kigeni kutoka Umoja huo kuingilia kati ili kushawishi upinzani ushiriki mazungumzo, bila kutoa masharti yoyote.

Mawaziri hao kutka mataifa wanachama wa Umoja wa Amerika ya Kusini, wamekutana katika ziara yao mjini Caracas na upinzani, wanafunzi , makundi ya kidini na haki za binadamu, na rais mwenyewe.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.