Pata taarifa kuu
SYRIA-UTURUKI-ISIL-KOBANE-Usalama

Wapiganaji wa IS waendelea kudhibiti baadhi ya maeneo ya Kobane

Siku moja baada ya wapiganaji wa Dola la Kiislam kudhibiti maeneo matatu mashariki mwa Kobane nchini Syria, mapigano yanaendela kurindima mashariki na kusini mwa mji huo karibu na mpaka wa Syria na Uturuki.

Raia huyu  wa kikurdi aangalia mapigano katika mji wa Kobane akiwa katika kijiji chaMursitpinar, kwenye mpaka wa Uturuki na Syria, Oktoba 6 mwaka 2014.
Raia huyu wa kikurdi aangalia mapigano katika mji wa Kobane akiwa katika kijiji chaMursitpinar, kwenye mpaka wa Uturuki na Syria, Oktoba 6 mwaka 2014. AFP PHOTO / ARIS MESSINIS
Matangazo ya kibiashara

Kwa mujibu wa shirika la haki za binadamu nchini Syria, muungano wa kimataifa umeendesha usiku wa jumatatu kuamkia leo jumanne mashambulizi mapya dhidi ya ngome za wapiganaji wa dola la Kiislam.

Ni wiki tatu sasa tangu mapigano kati ya wapiganaji wa Dola la Kiislam na wapiganaji wa Kiikurdi kuzuka karibu na mpaka wa Syria na Uturuki. Wapiganaji wa dola la Kiislam wametishia kuudhbiti mji wa Kobane.

Kwa mujibu wa kiongozi wa shirika la kutetea haki zabinadamu nchini syria, mapigano hayo kati ya wapiganaji wa Dola la Kiislam na wapiganaji wa kikurdi yameelekea kuwa mashambulizi ya kuvizia kwenye barabara za mji wa Kobane. Raia wameyahama makaazi yao na kukimbilia katika nchi jirani ya Uturuki. Kobane ni mji wa tatu unaokaliwa na watu kutoka jamii ya wakurdi wa Syria.

Hayo yakijiri, Bunge la Uturuki liliiruhusu Alhamisi serikali ya Ankara kuchukua uamzi wa kutuma majeshi yake nchini Syria na Iraq kwa lengo la kuendesha mashambulizi dhidi ya wapiganaji wa dola la Kiislam.

Barani Ulaya, kumekua na uhamasishaji wa haraka na wenye nguvu, hususan katika nchi za Ufaransa, ujerumani, Ubelgiji, Uholanzi. Denmark na Norway. Viwanja vya ndege vimefungwa, huku maandamano yakipangwa kufanyika ili kushinikiza mataifa hayo kupambana vilivyo kwa kuhofia kutekwa kwa mji wa Kobane na wapiganaji wa Dola la Kiislam.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.