Pata taarifa kuu
MEXICO-Haki za binadamu-Usalama

Hali ya taharuki yaendelea kutanda Mexico

Kesi ya mauaji ya wanafunzi Mexico 43 ambao wameripotiwa kupotea tangu yalipotokea makabiliano kati ya polisi na makundi ya wauza dawa za kulenvya mwezi uliopita, imechukua sura mpya baada ya kugunduliwa kwa kaburi jingine la pamoja.

Vicente Carrillo, kaka wa Amado Carrillo Fuentes, wakati akikamatwa, ambaye ni mmoja wa watuhumiwa wa mauwaji ya wanafunzi 43 nchni Mexico.
Vicente Carrillo, kaka wa Amado Carrillo Fuentes, wakati akikamatwa, ambaye ni mmoja wa watuhumiwa wa mauwaji ya wanafunzi 43 nchni Mexico. REUTERS/Edgard Garrido
Matangazo ya kibiashara

Habari hizi zimepokelewa kwa mshtuko na familia za wanafunzi waliopotea ambapo washukiwa wengine wanne waliwapeleka maofisa usalama kwenye eneo jingine ambalo wamedai watu zaidi wamezikwa kusini mwa jiji la Mexico huku idadi kamili ya miili ikiwa haijajulikana.

Uvumbuzi wa kaburi jingine la pamoja kunazima kabisa matumaini ya familia hizi kuwapata watoto wao wakiwa hai ikiwa ni wiki mbili toka polisi wanaotuhumiwa kuwa na uhusiano na makundi yenye silaha kudaiwa kutekeleza mauaji hayo.

Mwendesha mashtaka wa Mexico, Jesus Murillo Karam amewaambia waandishi jijini Mexico kuwa mpaka sasa ni washukiwa wawili pekee ndio wamekiri kuhusika na mauaji ya wanafunzi 17 kati ya 43 na kuwazika kwenye kaburi la pamoja mjini Guerroros.

Wachunguzi wa tukio hili wanadai kuwa makaburi manne zaidi yamegunduliwa ambapo miili ya wanafunzi hao, mingi imekutwa imekatwa baadhi ya sehemu ya viungo na mingine kuunguzwa.

Mpaka sasa ni miili 28 ambayo haijatambuliwa imeshapatikana wakati huu wazazi wa wanafunzi hao wakisubiri uchunguzi wa vinasaba.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.