Pata taarifa kuu
UJERUMANI-WAKIMBIZI-USALAMA

Ujerumani: zaidi ya watoto wakimbizi 8,000 watoweka

Zaidi ya wakimbizi milioni walipokelewa mwaka jana nchini Ujerumani. Miongoni mwao watoto wengi, watoto wadogo ambao hawakua na ndugu zao walitarajiwa kupata ulinzi wa ziada na msaada mkubwa.

Wahamiaji wa Eritrea wanane, ikiwa ni pamoja na watoto saba walikutwa salama katika lori lenye friji kaskazini mwa Ufaransa. (Picha zilizopigwa Idomeni, Machi 25, 2016).
Wahamiaji wa Eritrea wanane, ikiwa ni pamoja na watoto saba walikutwa salama katika lori lenye friji kaskazini mwa Ufaransa. (Picha zilizopigwa Idomeni, Machi 25, 2016). REUTERS/Marko Djurica
Matangazo ya kibiashara

Hata hivyo, maelfu miongoni mwao walitoweka. Wizara ya Mambo ya Ndani ya Ujerumani imetangaza takwimu ya wakimbizi watoto 8 629 waliotoweka Aprili 1, 2016.

Ofisi ya polisi ya Ulaya Europol, wiki chache zilizopita ilitoa idadi ya wakimbizi watoto 10,000 ambao wametoweka na hali hiyo tayari imeibua mijadala katika nchi wanachama. Wizara ya Jamii fnchini Ujerumani ilisema miezi miwili iliyopita kwamba haina taarifa kuhusu kutoweka kwa watoto hao.

Magazeti kadhaa yametoa ripoti Jumatatu hii Aprili 11ya jibu la Wizara ya Mambo ya Ndani kwa mbunge wa Ujerumani. Wakimbizi watoto 8629 walitoweka Aprili 1, wengi wao wakiwa na umri wa miaka iliyo kati ya 14 na 17. Serikali mbalimbali barani Ulaya zinaeleza ongezeko hilo limesababishwa naviongozi wenye uzowefu waliozidiwa na hali hiyo. Watoto ambao wamejiunga na familia zao mahali pengine nchini Ujerumani au nje ya nchi wataendelea kubaki kwenye orodha ya watoto waliotoweka.

Mwishoni mwa mwezi Machi, Wabunge wa Ulaya walibainisha hatari ya watoto kuwa waathirika wa magenge yaliyoandaliwa ambayo yanaweza kuwapelekea katika ukahaba, kufanya kazi au kutoa viungo vyao vya mwili. Mbunge wa Bunge la Ujerumani alieihoji Wizara ya Mambo ya Ndani anajiuliza iwapo Berlin inachukulia hatari hiyo kwa jambo la kawaida.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.