Pata taarifa kuu

Wamarekani wawili na Mdenmark watunukiwa Tuzo ya Nobel ya 2022 katika Kemia

Tuzo ya Nobel ya 2022 katika Kemia imetolewa Jumatano Oktoba 5 kwa raia wa Denmark Morten Meldal, Mmarekani Carolyn Bertozzi na raia mwenzake Barry Sharpless, ambaye ameweza kutunikiwa Tuzo ya Nobel ya pili ya kazi yake. Watatu hao wametunukiwa "kwa maendeleo ya 'kemia ya kubofya' na kemia ya bioorthogonal", imetangaza bodi ya Tuzo ya Nobel katika uamuzi wake.

Tuzo ya Nobel ya Kemia ya 2022 ilitolewa, Jumatano hii, Oktoba 5, kwa Wamarekani Carolyn R. Bertozzi na K. Barry Sharpless, pamoja na raia wa Denmark Morten Meldal.
Tuzo ya Nobel ya Kemia ya 2022 ilitolewa, Jumatano hii, Oktoba 5, kwa Wamarekani Carolyn R. Bertozzi na K. Barry Sharpless, pamoja na raia wa Denmark Morten Meldal. © AP/Christine Olsson
Matangazo ya kibiashara

Mtafiti wa Marekani Barry Sharpless, aliyeishi California, na raia wa Denmark mwenye umri wa miaka 58, Morten Meldal, wa Chuo Kikuu cha Copenhagen, wametunukiwa kwa kazi yao ya upainia katika "kemia ya kubofya" ambayo inafanya uwezekano wa kukusanya molekuli pamoja. Hii inatumika hasa kutengeneza matibabu ya dawa, ramani ya DNA au kuunda nyenzo mpya.

Barry Sharpless, 81, ni mtu wa tano tu kutunukiwa Tuzo ya Nobel mara mbili. Tayari alikuwa ameshinda tuzo ya kemia mnamo 2001 kwa uvumbuzi wake juu ya mbinu ya kichocheo cha asymmetric.

Mmarekani Carolyn Bertozzi, 55, ni ametunukiwa tuzo hiyo kwa uvumbuzi wa kemia ya bioorthogonal, mmenyuko wa kemikali unaoelezewa kuwa na uwezo wa kuanzishwa katika kiumbe hai, lakini bila kusumbua au kubadilisha asili yake ya kemikali. Anakuwa mwanamke wa nane kutunukiwa tuzo hii, akimrithi Mfaransa Emmanuelle Charpentier na Mmarekani Jennifer Doudna.

"Tuzo la mwaka huu katika kemia ni kuhusu mambo ambayo si magumu kupita kiasi," alisema Johan Åqvist, mmoja wa wajumbe wa kamati ya Nobel ya kemia.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.