Pata taarifa kuu
USHIRIKIANO-DIPLOMASIA

NATO: Blinken atoa wito kwa Uturuki na Hungary kuidhinisha uanachama wa Sweden 'bila kuchelewa'

Mkuu wa diplomasia ya Marekani Antony Blinken, siku ya Jumanne, ametoa wito kwa Uturuki na Hungary kuidhinisha "bila kuchelewa" kujiunga kwa Swedeni kwa NATO, muda mfupi baada ya kuingia rasmi kwa Finland katika Muungano wa Atlantiki.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken. AP - Petr David Josek
Matangazo ya kibiashara

"Tunahimiza Uturuki na Hungary kuidhinisha itifaki za Sweden kujiunga kwa NATO bila kuchelewa ili tuweze kukaribisha Sweden katika Muungano wa Atlantiki haraka iwezekanavyo," amesema katika taarifa iliyotolewa katika sherehe ya kuondoa bedera ya Finland kwenye makao makuu ya NATO huko Brussels.

Uturuki inazuia uwanachama wa Sweden, inayoshutumiwa kwa kutokuwa na adabu mbele ya "magaidi" wa Kikurdi ambao wamekimbilia katika nchi hii na inadai warejeshwe wakati serikali haina neno la mwisho. Hungary, kwa upande wake, inaishtumu Sweden kwa ukosoaji wake kwa serikali ya Viktor Orban, inayotuhumiwa kutoheshimu utawala wa sheria.

Katibu Mkuu wa NATO Jens Stoltenberg amesema, "Sweden imetimiza ahadi zote ambazo zimeombwa." "Washirika wote wanatarajia mchakato wa Sweden kujiunga na NATO kukamilika haraka iwezekanavyo. Hiki ni kipaumbele kwa Muungano", amesisitiza mwanzoni mwa mkutano wa mawaziri wa mambo ya nje wa NATO.

Antony Blinken amekutana Jumanne uso kwa uso na mkuu wa diplomasia ya Uturuki Mevlut Cavusoglu. Lithuania, ambayo inaandaa mkutano ujao wa NATO mnamo mwezi Julai huko Vilnius, inatumai kuwa Sweden itakuwa imejiunga ifikapo tarehe hiyo.

"Tunatumai kuwa bendera ya Sweden itapepea katika NATO kwa mkutano wa Vilnius," Waziri wa Mambo ya Nje wa Lithuania Gabrielius Landsbergis amesema. "Natoa wito kwa Rais Erdogan kutoharibu mkutano wa Vilnius," amesema.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.