Pata taarifa kuu

India yaweka historia kupeleka chombo cha uchunguzi mwezini

NAIROBI – Chombo cha uchunguzi wa anga cha India, hatimaye kimetua salama mwezini, ambapo taifa hilo linakuwa la kwanza kufanya hivyo, siku chache baada ya chombo cha Urusi, kuharibika na kusambaratika dakika chache kabla ya kutua.

India kwa mara ya kwanza imetua mwezini kwa mafanikio.
India kwa mara ya kwanza imetua mwezini kwa mafanikio. AP - Aijaz Rahi
Matangazo ya kibiashara

Akifuatilia kutoka Afrika Kusini, Waziri mkuu, Narendra Modi, amepongeza mafanikio hayo ambayo yametajwa kama hatua kubwa kwa taifa hilo la Asia.

Awali wanasiasa nchini humo walikuwa wamefanya maombi ya kitamaduni wakiwa na matumaini ya kufanikisha hatua hiyo ambayo imefuatiliwa na maelfu ya raia wa nchi hiyo.

Nchi hiyo yenye idadi kubwa ya watu duniani, ilifanya jaribio lingine ambalo halikufanikiwa mwaka 2019.

Mamlaka ya kuchunguza masuala ya anga nchini humo, ilikuwa  imefanya maboresho zaidi kwa chombo hicho ili kuepuka kilichotokea miaka minne iliyopita wakati wanasayansi walipoteza mawasiliano na chombo chao kabla ya kutua.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.