Pata taarifa kuu

Bei bei za vyakula zilipungua kwa asilimia 13.7 mwaka wa 2023: FAO

Nairobi – Besi ya chakula duniani iliripotiwa kuchuka mwaka 2023, huku wasiwasi uliokuwepo kuhusu upatikanaji wa ngano na nafaka ukipungua, imesema ripoti ya shirika la chakula na kilimo, FAO.

Wakati hofu ya upatikanaji wa ngano na mahindi ikipungua, ilikuwa kinyume kwa mchele kutokana na athari za hali ya hewa ya El Nino
Wakati hofu ya upatikanaji wa ngano na mahindi ikipungua, ilikuwa kinyume kwa mchele kutokana na athari za hali ya hewa ya El Nino REUTERS - Daniel Acker
Matangazo ya kibiashara

Kwa mujibu wa FAO, kiujumla bei za vyakula zilipungua kwa asilimia 13.7 katika mwaka wa 2023 ikilinganishwa na ilivyokuwa katika kipindi cha mwaka uliotangulia.

Wakati hofu ya upatikanaji wa ngano na mahindi ikipungua, ilikuwa kinyume kwa mchele kutokana na athari za hali ya hewa ya El Nino, huku India mzalishaji mkubwa wa nafaka hiyo ikipunguza uuzaji wa nje, ambapo bei iliongezeka kwa asilimia 21 mwaka uliopita.

Katika taarifa yake, FAO inasema kuwa usambazaji wa nafaka uliongoezeka katika masoko mwaka 2023 hatua ambayo ilipunguza kwa asilimia kubwa uhitaji wa bidhaa za chakula.

Hata hivyo wakati ripoti ya FAO ikionesha kiujumla kupunguia kwa bei za bidhaa za chakula, raia kwenye mataifa mengi wameendelea kushuhudia ongezeko la bei hata zaidi ya kiwango cha mfumuko wa bei, hali hii ikichangiwa pakubwa na ongezeko la gharama za nishati na wafanyakazi wakati wa usindikaji na usambazaji.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.