Pata taarifa kuu

Uganda yatoa leseni ya ujenzi wa bomba la mafuta lenye utata

Uganda imetoa leseni ya ujenzi wa bomba la mafuta linalovuka nchi hiyo na Tanzania, linalokusudiwa kusafirisha madini ya hidrokaboni kutoka Afrika Mashariki hadi katika masoko ya kimataifa, jambo ambalo limeibua hasira za wanaharakati wa mazingira.

Rais wa Uganda Yoweri Museveni mnamo Januari 16, 2022, katika makazi yake huko Kisozi.
Rais wa Uganda Yoweri Museveni mnamo Januari 16, 2022, katika makazi yake huko Kisozi. REUTERS - ABUBAKER LUBOWA
Matangazo ya kibiashara

"Kuidhinishwa (kwa leseni) ni ishara nyingine ya kuonyesha dhamira ya pamoja ya nchi hizo mbili kuendeleza mradi wa EACOP kwa njia iliyowiana," Waziri wa Habari wa Uganda Godfrey Kabbyanga aliliambia shirika la habari la AFP siku ya Ijumaa.

Leseni hiyo ilitolewa kwa muungano wa East African Crude Oil Pipeline Company Ltd (EACOP), asilimia 62 inayomilikiwa na kampuni kubwa ya Ufaransa ya TotalEnergies, kufuatia idhni liotolewa na serikali ya Uganda siku ya Jumatatu.

Kampuni ya TotalEnergies ilitangaza mwezi Februari mkataba wa uwekezaji wa dola bilioni 10 na Uganda, Tanzania na kampuni ya China ya CNOOC, ikiwa ni pamoja na ujenzi wa bomba la mafuta la kilomita 1,443 (EACOP) linalounganisha visima vya Ziwa Albert, magharibi mwa Uganda, na pwani ya Tanzania kwenye Bahari ya Hindi.

Mradi huo, hata hivyo, umepata upinzani kutoka kwa wanaharakati wa mazingira na vikundi vinavyoamini kuwa unatishia mfumo wa ikolojia dhaifu wa eneo hilo na watu wanaoishi huko.

Mashirika sita yasiyo ya kiserikali yaliishtaki TotalEnergies mbele ya mahakama ya Paris mwishoni mwa mwaka 2022, na kulitaka kundi hilo kuheshimu sheria iliyopitishwa mwaka wa 2017 ambayo inalazimisha mashirika ya kimataifa "wajibu wa kukesha" kwa shughuli zao duniani. Majadiliano hayo yanatarajiwa tarehe 28 Februari.

Ziwa Albert, mpaka wa asili kati ya Uganda na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, lina wastani wa mapipa bilioni 6.5 ya mafuta yasiyosafishwa, ambapo takriban mapipa bilioni 1.4 yanachukuliwa kuwa yanaweza kurejeshwa. Tone la kwanza la mafuta ya Uganda linatarajiwa kutiririka mwaka 2025, karibu miongo miwili baada ya hifadhi kugunduliwa.

Rais Yoweri Museveni anatarajiwa kuhudhuria uzinduzi wa shughuli za uchimbaji visima katika visima vya mafuta vya Kingfisher vinavyoendeshwa na CNOOC katika Ziwa Albert siku ya Jumanne. Bw. Museveni alielezea mradi huo kama chanzo kikuu cha kiuchumi kwa nchi hii isiyo na bahari, ambapo watu wengi wanaishi katika umaskini.

Uganda itakuwa mwenyeji wa Kongamano la 10 la Petroli la Afrika Mashariki kuanzia Mei 9-11 ili kuonyesha Afrika Mashariki kama "eneo kuu la uvumbuzi wa hidrokaboni", Kabbyanga alisema. Serikali pia inafanya tafiti ili kufungua maeneo mengine ya nchi kwa utafutaji wa mafuta, aliongeza.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.