Pata taarifa kuu
USALAMA-JAMII

Uganda: Watatu wauawa, wakiwemo watalii wawili wa kigeni, katika shambulio

Watu watatu, wakiwemo watalii wawili wa kigeni, wameuawa na watu wenye silaha katika Mbuga ya kitaifa ya Malkia Elizabeth, polisi imetangaza siku ya Jumanne, Oktoba 17, ikihusisha shambulio hilo na kundi la waasi. "Watu hao watatu waliuawa na gari lao kuchomwa moto," msemaji wa polisi Fred Enanga amesema kwenye X (zamani ikiitwa Twitter).

Gari la jeshi la Uganda limeegeshwa chini ya mlima wa Rwenzori, karibu na mji wa Kichwamba (kusini-magharibi mwa Uganda), umbali wa kutupa jiwe kutoka DRC, mnamo Desemba 2015.
Gari la jeshi la Uganda limeegeshwa chini ya mlima wa Rwenzori, karibu na mji wa Kichwamba (kusini-magharibi mwa Uganda), umbali wa kutupa jiwe kutoka DRC, mnamo Desemba 2015. Gaël Grilhot/RFI
Matangazo ya kibiashara

Kundi hilo la watali lilikuwa likitembea kwenye Mbuga ya kitaifa ya Malkia Elizabeth liliposhambuliwa na wanamgambo wa Allied Democratic Forces (ADF), msemaji wa polisi amesema. "Vikosi vyetu vilijibu mara tu baada ya kufahamishwa kuhusu shambulio hilo na vinawasaka kwa udi na uvumba washukiwa ambao ni waasi wa ADF," ameongeza.

Uraia wa watalii haukutajwa lakini mwathirika wa tatu ni Mganda.

Hapo awali waasi hao wa Uganda ambao wengi wao ni Waislamu, wanaoendesha harakati zao nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) tangu miaka ya 1990, ambao walitangaza mwaka wa 2019 kuwa wanajiunga na kundi la Islamic State, ambalo linakiri kutekeleza baadhi ya vitendo vyao viovu na kulichukulia kundi la ADF  kama tawi lao Afrika katikati" (Iscap kwa Kiingereza). Wanatuhumiwa kuua maelfu ya raia katika kipindi cha miaka kumi iliyopita.

Katika ripoti yake ya hivi punde iliyochapishwa mwezi Juni, kundi la wataalamu wa Umoja wa Mataifa kuhusu DRC linasema kuwa IS "imetoa msaada wa kifedha kwa ADF tangu angalau mwaka 2019, kupitia mfumo tata wa kifedha unaohusisha watu binafsi katika nchi kadhaa barani Afrika, zinazotoka Somalia na kupitia Afrika Kusini, Kenya na Uganda.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.