Pata taarifa kuu

Kufukuzwa kwa wahamiaji kwenda Rwanda: Kigali 'imeridhika' na kura ya Bunge la Uingereza

Serikali ya Kigali "imeridhishwa" siku ya Jumanne na kura ya Bunge la Uingereza kuhusu mswada wenye utata unaoruhusu kufukuzwa kwa waomba hifadhi walioingia nchini Uingereza kinyume cha sheria na kupelekwa nchini Rwanda, amesema msemaji wa serikali ya Rwanda. 

Upande wa kushoto, Waziri wa Mambo ya Ndani wa Uingereza James Cleverly akipeana mkono na Waziri wa Mambo ya Nje wa Rwanda Vincent Biruta baada ya kusainiwa kwa mkataba mpya wenye utata mjini Kigali siku ya Jumanne, Desemba 5, unaolenga kuwafukuza wahamiaji waliongia nchini Uingereza kinyume cha sheria na kupelejwa nnchini Rwanda.
Upande wa kushoto, Waziri wa Mambo ya Ndani wa Uingereza James Cleverly akipeana mkono na Waziri wa Mambo ya Nje wa Rwanda Vincent Biruta baada ya kusainiwa kwa mkataba mpya wenye utata mjini Kigali siku ya Jumanne, Desemba 5, unaolenga kuwafukuza wahamiaji waliongia nchini Uingereza kinyume cha sheria na kupelejwa nnchini Rwanda. via REUTERS - POOL
Matangazo ya kibiashara

"Tumeridhika kwamba mswada huo umepitishwa na Bunge la Uingereza," Yolande Makolo amesema katika taarifa iliyotumwa kwa shirika la habari la AFP, akiongeza kuwa mamlaka "zina hamu ya kuwapokea watu waliohamishwa kwenda Rwanda".

Hata hivyo Baraza la Umoja wa Ulaya (EU) na Umoja wa Mataifa wameitaka Uingereza kurejelea sheria yake.

Mkuu wa Haki za Binadamu katika Barazala la Umoja wa Ulaya ametoa wito leo Jumanne kwa serikali ya Uingereza kurejelea muswada huu wa sheria wa kuwafukuza wahamiaji kwenda nchini Rwanda, baada ya mabunge mawili kupigia kura muswada huo.

"Serikali ya Uingereza inapaswa kujizuia kuwafukuza watu kufuatia mpango wake wa kuwapeleka nchini Rwanda na kurejelea kuhusu ukiukwaji wa uhuru wa mahakama dhidi ya muswada huo wa sheria ", amesema Mkuu wa Haki za Binadamu kwenye Baraza la Ulaya, Michael O’Flaherty. London ni sehemu ya taasisi hii inayoundwa na nchi 46 wanachama.

Umoja wa Mataifa umetoa wito kama , ukiitaka serikali ya Uingereza kurejelea mpango wake wa kuwafukuza waomba hifadhi na kuwapeleka nchini Rwanda.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.