Pata taarifa kuu

DRC: Vital Kamerhe ameteuliwa kugombea nafasi ya spika kupitia sacred unión

Kiongozi wa chama cha UNC na mshirika wa karibu wa rais wa Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo Vital Kamerhe ameteuliwa kama mgombea pekee wa kiti cha spika wa bunge ambaye atapeperusha bendera ya muungano wa kitaifa unaofahamika kama sacred unión.

Vital Kamerhe ameteuliwa kama mgombea pekee wa kiti cha spika wa bunge ambaye atapeperusha bendera ya muungano wa kitaifa unaofahamika kama sacred unión.
Vital Kamerhe ameteuliwa kama mgombea pekee wa kiti cha spika wa bunge ambaye atapeperusha bendera ya muungano wa kitaifa unaofahamika kama sacred unión. © AFP - FABRICE COFFRINI
Matangazo ya kibiashara

Wafuasi wake kutoka chama cha UNC walijawa na furaha punde baada ya kiongozi wao Vital Kamerhe kutangazwa mshindi wa uchaguzi wa spika wa bunge la taifa siku ya Jumanne Jijini Kinshasa.

Mwanasiasa huyo mwenye umaarufu sana huko DRC alishinda kura 183 kati ya wapiga kura 372, wengi wao wakiwa ni wabunge kutoka muungano unaotawala chini ya rais Felix Tshisekedi Union sacrée de la Nation.

Vital Kamerhe ni mshirika wa karibu wa rais wa DRC Felix Tshisekedi katika muungano watakatifu.
Vital Kamerhe ni mshirika wa karibu wa rais wa DRC Felix Tshisekedi katika muungano watakatifu. AFP - ALEXIS HUGUET

Akizungumza kabla ya wabunge kupiga kura, katibu Mkuu wa chama tawala cha UDPS Augustin Kabuya alisema kuwa Muungano wao huo unaotawala, ulishindwa kuja na jina moja la mgombea wa nafasi hiyo kati ya wagombea watatu wakiwemo Modeste Bahati ambaye alikuwa spika wa senate, Christophe Mboso alikuwa spika wa bunge la taifa naye Vital Kamerhe.Punde baada ya kuteuliwa kwake, Kamerhe alisema:

“Yani sisi tutakuwepo tukiwa waaminifu kwa rais wa Jamhuri ya kidemokrasia ya Kongo na kumpa pumzi mpya pia kuondoa mashaka yote sababu tangu mwanzo tumekuwa pamoja.” alisema Vital Kamerhe.

Christophe Mboso alipata kura 113 huku Modeste Bahati akichaguliwa kwa kura 69 pekee. Kura saba zilitangazwa kuwa batili.

Christophe Mboso spika wa bunge lilopita alikuwa miongoni mwa waliokuwa wanataka kuwania nafasi hiyo.
Christophe Mboso spika wa bunge lilopita alikuwa miongoni mwa waliokuwa wanataka kuwania nafasi hiyo. AFP - ARSENE MPIANA

Matarajio ya wananchi huko DRC ni kuyaona mabadiliko katika hali ya maisha na kurejea kwa usalama wa mashariki mwa nchi hiyo.

RFI.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.