Pata taarifa kuu
UGANDA-UNHCR-WAKIMBIZI-CORONA-AFYA

UNHCR yatiwa na wasiwasi na hali ya wakimbizi nchini Uganda

Shirika la Umoja wa Mataifa linalowashughulikia wakimbizi linasema maisha ya Mamilioni ya wakimbizi wanaoishi nchini Uganda yapo hatarini kwa sababu Shiirika hilo halina fedha kukidhi mahitaji yao, kutokana na janga la virusi vya Corona.

Kufikia sasa Uganda imerekodi visa 774 vya maambukizi ya Corona, huku wagonjwa 631wakithibitishwa kupona. Hakuna kifo chochote kinachohusiana na Covid-19 kimeripotiwa nchini humo.
Kufikia sasa Uganda imerekodi visa 774 vya maambukizi ya Corona, huku wagonjwa 631wakithibitishwa kupona. Hakuna kifo chochote kinachohusiana na Covid-19 kimeripotiwa nchini humo. (c) Epicentre
Matangazo ya kibiashara

Serikali ya Uganda, kupitia waziri wake anayesimamia maswala ya wakimbizi Hillary Onek, imesema Jumuiya ya kimataifa inapaswa kuimarisha juhudi zake kusaidia wakimbizi au wengi watarudishwa kwa nchi zao.

Serikali ya Uganda pia imethibitisha kesi za Covid-19 kati ya wakimbizi.

Kufikia sasa Uganda imerekodi visa 774 vya maambukizi ya Corona, huku wagonjwa 631wakithibitishwa kupona. Hakuna kifo chochote kinachohusiana na Covid-19 kimeripotiwa nchini humo.

Waziri anayesimamia maswala ya wakimbizi Hillary Onek amesema kuna hatua ambazo zimechukuliwa kwa kuzuia maambukizi zaidi miongoni mwa wakimbizi

Serikali ya Uganda ambayo ilikuwa imeacha kuruhusu wakimbizi wapya katika maeneo yake tangu kutokea ugonjwa wa Covid-19 imeamua kuruhusu wakimbizi zaidi ya 4000 kutoka DRC kungia inchini. Shirika la Wakimbizi UNHCR wanaomba pesa zaidi ili kuondoa mzozo unaoweza kutokea kwa utunzaji wa wakimbizi .

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.