Pata taarifa kuu
MALAYSIA-UKRAINE-Ajali ya ndege

Ndege ya Malaysia yadunguliwa katika anga ya Ukraine

Ndege ya Malaysia iliyokuwa inatokea Amsterdam kuelekea Kuala Lumpur, nchini Malaysia, imeangushwa kwa kombora kwenye anga la nchi ya Ukraine ikiwa na abiria wasiopungua 298, zaidi ya nusu ya abiria hao wakiwa waholanzi.

Mabaki ya ndege Boeing 777 ya Malaysia Airlines iliypata ajali alhamisi Julai 17 mwaka 2014
Mabaki ya ndege Boeing 777 ya Malaysia Airlines iliypata ajali alhamisi Julai 17 mwaka 2014 REUTERS/Maxim Zmeyev
Matangazo ya kibiashara

Wataalam kutoka Marekani wanaamini kwamba ndege hiyo aina ya Boeing 777 imerushiwa kombora katika eneo la mashariki linalodhibitiwa na waasi wanaounga mkono urusi, jambo ambalo limesababisha shutma kuelekea upande mwengine wa mahasimu hao kama alivyobainisha rais wa Ukraine Petro Poroshenko.

“Nimewaalika wataalamu wa Uholanzi kubaini kilichotokea na kuanzisha uchunguzi kwa tukio hili la kigaidi. Nigetamani kuwaambia kuwa katika hili hatuoni kuwa ni ajali, lakini ini ugaidi”, amesema Poroshenko.

Kwa upande wa serikali ya malaysia, jambo hilo ni la kuhuzunisha na kuomba uchunguzi ufanyike haraka iwezekanavyo kubaini wahusika wa tukio hilo kwa vile wanaamini kuwa sio ajali.

“Nimepokea simu kutoka kwa rais wa Marekani, Barack Obama na tumekubaliana uuanzisha uchunguzi wa kina na uchunguzi huo haupaswi kuzuiwa na kwa njia yoyote ile. Timu ya kimataifa ya uchunguzi itafanya jukumu hilo kwa uhuru na haipaswi kuingiliwa na mtu yoyote, hata eneo la ajali hakuna mtu anyeruhusiwa kuondoa kitu chochote kikiwemo kisanduku cha taarifa ya ndege. Hili ni janga na hakika hili ni janga kwa wananchi ya Malaysia”, amesema waziri mkuu wa Malaysia Najib Mansouri.

Waasi wa Ukriane wanaoungwa mkono na Urusi wamesema wako tayari kuruhusu uchunguzi wa kimataifa uanzishwe kwenye eneo la tukio ili kubainika sababu za ajali ya ndege hio, Jumuiya ya Usalama na Ushirikano barani Ulaya (OSCE) imethibitisha.

Ajali hii ni ya pili inayolikumba shirika la ndege la Malaysia Airlines kwa kipindi kisiyozidi miezi 5. Ndege nyingine aina ya Boeing 777 ya Malaysia Airlines iliopotea usiku wa tarehehe 7 kuamkia 8 Machi mwaka huu ikiwa na abiria 227, na hadi wakati huu ndege hiyo haijapatikana.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.