Pata taarifa kuu
PALESTINA-ISRAELI-MISRI-HAMAS-Usalama

Palestina : mke na mtoto wa kiongozi wa kijeshi wa Hamas wauawa

Kundi la Hamas nchini Palestina limethibitisha kuwa shambulio la anga lililotekelezwa na ndege za Israel usiku wa kuamkia leo kwenye eneo la ukanda wa Gaza limeua mke na mtoto wa kiongozi wa kijeshi wa kundi hilo, Mohammed Deif.

Jeshi la Israeli linaendelea na mashambulizi ya anga katika ukanda wa Gaza.
Jeshi la Israeli linaendelea na mashambulizi ya anga katika ukanda wa Gaza.
Matangazo ya kibiashara

Naibu kiongozi wa kundi la Hamas anayeishi uhamishoni, Mussa Abu Marzuk, ameandika kwenye mtandao wake wa kijaamii wa Facebook kuuawa kwa familia ya kiongozi wa kijeshi wa Ezzedine al-Qassam bila kusema iwapo nae aliuawa kwenye shambulio hili.

Tukio hili limetekelezwa wakati huu ambapo mazungumzo kati ya kundi hilo na serikali ya Israel yakionekana kukwama mjini Cairo Misri baada ya kila upande kumshutumu mwenzake kwa kukikuka makubaliano ya kuendelea kusitisha mapigano.

Kundi la Hamas limethibitisha kurusha roketi kuelekea uwanja wa ndege wa Tel-Aviv nchini Israel huku likiapa kulipiza kisasi kufuatia mauaji hayo.

Waziri mkuu Benjamini Netanyahu ameendelea kujikuta kwenye shinikizo toka ndani ya chama chake na nje huku baadhi wakitaka jeshi la nchi hiyo liingie zaidi kwenye eneo la ukanda wa gaza kuwanyang'anya silaha wapiganaji wa Hamas.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.