Pata taarifa kuu
IRAQ-MAREKANI-ISLAMIC STATE-Usalama

Iraq: Marekani yashambulia ngome za wapiganaji wa Islamic State

Mashambulizi ya kwanza ya Marekani dhidhi ya ngome za kundi la IS yametekelezwa karibu na mji mkuu Bagdad nchini Iraq. Duru za kuaminika zimearifu kuwa mashambulizi 160 tayari yametekelezwa katika eneo la kusini magharibi mwa Mji huo.

Wapiganaji wa Peshmergas wakiangalia moshi unaotokana na mashambulizi ya anga ya jeshi la Marekani katika mji wa Makhmur, nchini Iraq.
Wapiganaji wa Peshmergas wakiangalia moshi unaotokana na mashambulizi ya anga ya jeshi la Marekani katika mji wa Makhmur, nchini Iraq. REUTERS/Azad Lashkari
Matangazo ya kibiashara

Kulingana na taarifa ya uongozi wa jeshi la Marekani katika ukanda mashariki ya kati Mashambulizi hayo yamelenga ngome za kundi la Islamic State katika eneo la kaskazini magharibi na yalilenga kulisaidia jeshi la Iraq katika mapambano dhidi ya wanamgambo hao.

Mashambulizi mengine ya anga yametekelezwa pia katika eneo la kaskazini karibu na mji wa Sinjar na kuharibu magari sita ya kijeshi ya kundi la IS.

Tangu Agosti 8 mwaka huu jeshi la Marekani linaendesha mashambulizi dhidi ya wapiganaji wa kundi la Islamic State ambao wameendelea kuwa tishio kwa usalama wa ukanda wa mashariki ya kati na ambo wamekalia maeneo kadhaa ya Iraq na Syria.

Rais Obama alitangaza hibi karibuni kuwa tayari kutekeleza mashambulizi dhidi ya ngome za IS nchini Syria huku akitupilia mbali hatuwa yoyote ya ushirikiano wa Marekani na serikali ya Damascus ambayo amesema imepoteza uhalali katika kulipiga vita kundi hilo. Hadi leo hakuna shambulizi lolote lililotekelezwa na Marekani dhidi ya kundi hilo nchini Syria.

Hayo yanajiri wakati jumuiya ya kimataifa katika kikao kilichofanyika jijini Paris nchini Ufaransa ikikubaliana na mpango wa Marekani kuungana katika kuisaidia Irak kwa njia zote zikiwemo za kijeshi katika harakati zake za kupambana na wanajihadi wa kundi la Islamic State bila hata hivyo kutaja hatuwa zilizochukuliwa dhidi ya kundi hilo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.