Pata taarifa kuu
UFARANSA-ISLAMIC STATE-Usalama-Diplomasia

François Hollande: “ hakuna muda wa kupoteza dhidi ya Islamic State”

Muungano wa kimataifa unajiandaa kupambana na kundi la wapiganaji wa kiislam la Islamic State. Ndege za kivita za Ufaransa zimefanya majaribio ya kukagua kwenye anga ya Iraq. Wakati huohuo, wawakilishi wa nchini 26 wanakutana mjini Paris ili kujadili mbinu zinazopaswa kutumiwa dhidi ya wapiganaji hao.

Rais wa Iraq, Fouad Mssoum akiwa na mwenyeji wake wa Ufaransa, François Hollande katika mkutano uhusuo amani na usalama kwa Iraq
Rais wa Iraq, Fouad Mssoum akiwa na mwenyeji wake wa Ufaransa, François Hollande katika mkutano uhusuo amani na usalama kwa Iraq REUTERS/Christian Hartmann
Matangazo ya kibiashara

Rais wa Ufaransa François Hollande ametangaza katika ufunguzi wa mkutano huo kwamba hawana muda wa kupoteza dhidi ya wapiganaji wa Islamic State. Kwa upande wake rais wa Iraq, Fouad Massoum ameutaka muungano wa kimataifa kuanzisha mashambulizi ya kimataifa haraka iwezekanavyo.

Mawakilishi wa mataifa 26 na mashirika 3 ya kimataifa wanashiriki katika mkutano huo ambao umeanza na shughuli mbalimbali katika wizara ya mambo ya nje ya Ufaransa. Waziri wa Ufaransa mwenye dhamana ya mambo ya nje, Laurent Fabius, anatazamiwa kutamatisha mkutano huo.

Katika mkutano huo, wanashiriki mawaziri wa mambo ya nje wa Marekani, John Kerry, Wa Urusi Serguei Lavrov, wa Saudia Arabia, wa Uturuki, Jordan pamoja na mawaziri wa mambo ya nje wa Ulaya. Rais wa Ufaransa amewatolea wito wafadhili wa kimataifa kushirikiana vilivyo na viongozi wa Iraq.

“ Islamic State ni tishio kwa ulimwengu, tunapaswa kuchukua hatua zinazohitajika kwa kutokomeza kundi hilo. (...) Umoja unahitajika kwa kuendesha katika ulimwengu huu. Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa katika azimio lake la 2170, limetangaza kuwa Daesh ni tishio kwa usalama wa dunia, Vita vinavyoendeshwa na Iraq dhidi ya magaidi inatuhusu”, amesema François Hollande.

Rais François Hollande, amebaini pia kwamba Ufaransa itashiriki katika vita dhidi ya wapiganaji wa Islamic State, lakini bila hata hivo kutoa taarifa zaidi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.