Pata taarifa kuu
ISRAEL-PALESTINA-UN-Usalama

Netanyahu hakubaliani na kuundwa kwa taifa la Palestina

Waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu amesema kuwa nchi yake kamwe haitakubali kutambua Mamlaka ya Palestina kama taifa huru kama ambavyo Mamlaka ya Palestina yamekuwa yakiuomba Umoja wa Mataifa kupitia Baraza la Usalama la Umoja huo.

Benjamin Netanyahu
Benjamin Netanyahu France 24
Matangazo ya kibiashara

Kauli hiyo ya Serikali ya Israel inakuja muda mfupi baada ya kuwasilishwa kwa azimio la kutaka kufanyika makubaliano ya mwisho kabla ya kutambulika rasmi kwa Palestina kuwa taifa kamili na huru.

Taarifa kutoka katika ofisi ya Benjamin Netanyahu imemtuhumu rais wa Mamlaka ya Palestina Mahmud Abbas kuwa hatua yake hiyo ya kutaka taifa la Palestina inalenga kuleta mkanganyiko na kuwapa nafasi kundi la Hamas.

Hayo yanajiri wakati huu Waziri wa Mambo ya kigeni wa Marekani, John Kerry, akitoa kauli ya kuashiria kuwa kuna umuhimu kwa Palestina kuwa taifa huru kwa njia ya mazungumzo ya amani.

Rasimu ya azimio la Palestina liliwasilishwa katikati ya juma hili kwenye Umoja wa Mataifa mjini New york nchini Marekani, ambapo pamoja na mambo mengine rasimu hiyo inapendekeza Israel iwe imeondoka katika himaya ya Mamlaka ya Palestina ifikapo mwaka 2017.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.