Pata taarifa kuu
ISRAELI-SIASA

Netanyahu afanikiwa kuunda serikali ya umoja

Waziri mkuu wa Israel amefanikiwa kuunda serikali ya umoja kutoka vyama tofauti. Netanyahu amefanikisha zoezi hilo kabla ya masaa mawili ya tarehe ya mwisho iliyopangwa kumalizika.

Benyamin Netanyahu na Naftali Bennett,kiongozi wa chama cha jamii ya Wayahudi, katika mkutano uliyofanyika Knesset, Mei 6 mwaka 2015.
Benyamin Netanyahu na Naftali Bennett,kiongozi wa chama cha jamii ya Wayahudi, katika mkutano uliyofanyika Knesset, Mei 6 mwaka 2015. AFP PHOTO / GALI TIBBON
Matangazo ya kibiashara

Waziri mkuu wa Israel amehitimisha mkataba na chama chenye msimamo mkali cha jamii ya Wayahudi, na hivyo kupata idadi ndogo ya wabunge.

Benjamin Netanyahu ameokoa wadhifa wake, baada ya kuafikiana kuungana na chama chenye msimamo mkali cha jamii ya Wayahudi na kumpelekea kuendelea kushikilia wadhifa wake wa Waziri mkuu. Vinginevyo, angelikua amepoteza nafasi yake, wakati huo rais wa Israel angelikabidhi majukumu hayo ya kuunda serikali kwa mtu mwengine.

Waziri mkuu ameunda muungano wa serikali, lakini kwa gharama zipi? Chama chenye msimamo mkali cha jamii ya Wayahudi kimekubali kuungana na chama cha Benjamin Netanyahu cha Likud, baada ya kukubaliwa kupewa nyadhifa muhimu katika serikali inayotarajiwa kuundwa. Kwa mujibu wa vyombo vya habari vya Israel, chama hicho kinapaswa kupata wizara kadhaa muhimu. Chama hicho cha mrengo wa Kati-Kulia kina mfumo wa Uzalendo na Dini. Chama hiki kinatetea ukoloni na kinapinga kuundwa kwa taifa la Palestina.

Muungano huu mpya pia utawaleta pamoja wajumbe wa chama cha Likud cha Benjamin Netanyahu, vyama viwili vya Ultra-Orthodox, kundi la wanaharakati wenye msimamo wa kati. Lakini muungano huo utakua na idadi ndogo ya wabunge, kura moja tu.

Benjamin Netanyahu, ambaye alishinda uchaguzi wa wabunge wa Machi 17, amekua akizungumza na vyama kadhaa vya kisiasa tangu mwezi mmoja na nusu uliyopita kwa minajili ya kujiunga na muungano wake. Lakini majadiliano yamekua magumu zaidi kuliko ilivyotarajiwa.

Baada ya uchaguzi, Benjamin Netanyahu aliahidi kuunda muungano katika kipindi cha wiki tatu. Mwezi mmoja na nusu baadaye umekamilika, mungano huo ukiwa bado haujaundwa. Waziri Mkuu, ambaye hangeliweza kutawala na chama chake pekee cha Likud, kutokana na kushindwa kupata wabunge wengi katika Baraza la Bunge.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.