Pata taarifa kuu
IRAN-NYUKLIA-USALAMA-DIPLOMASIA

Mkataba kuhusu mpango wa nyukila wa Iran wasainiwa

Rais wa Iran Hassan Rohani amesema kuwa mkataba ulisainiwa Jumanne asubuhi wiki hii katika mji wa Vienna unatamatisha " vikwazo visio halali na visio eleweka" na vitapelekea kuwepo na "kasi mpya" katika uhusiano kati ya Iran na nchi " 5 + 1 " zenye nguvu.

Mazungumzo ya mkataba kuhusu mpango wa nyuklia wa Iran wakati wa tangazo la kutia saini kwenye mkataba,Jumanne Julai 14.
Mazungumzo ya mkataba kuhusu mpango wa nyuklia wa Iran wakati wa tangazo la kutia saini kwenye mkataba,Jumanne Julai 14. REUTERS/Joe Klamar/Pool
Matangazo ya kibiashara

Nchini Iran raia wamepokea vema tangazo la kusitishwa hivi karibuni vikwazo vya kiuchumi.

Rais Rohani amezungumza kwenye televisheni baada ya kutangazwa kwa kusainiwa kwa mkataba katika mji wa Vienna siku ya Jumanne asubuhi wiki hii. Kwa upande wake, mkataba huu unaashiria " mwisho na mwanzo ": " mwisho wa vikwazo visio halali na visio eleweka dhidi ya raia wa Iran na ni mwanzo wa enzi mpya, kwa ajili ya ushirikiano wa kimataifa. "

“ Kama mkataba huu umefikiwa kwa mujibu wa sheria, tunaweza hatua kwa hatua kujenga imani ”, amesema rais Rhani.

Katika mji wa Tehran, hakujashuhudiwa mlipuko wa furaha. Viongozi wa Iran wamechukua hata hivyo hatua na kupeleka vikosi vya usalama katika maeneo kwa kuhofia kutokea mashambulizi mbalimbali wakati wa kutia saini kwenye mkataba huo. Mikusanyiko ya watu inatazamiwa kufanyika baadaye Jumanne jioni.

Vikwazo ambavyo viligharimu dola bilioni 200

Kuondolewa kwa vikwazo baada ya kutiliwa saini kwenye mkataba ni furaha kwa nchi ya Iran ambayo itaonekana kupumua zaidi baada ya kubanwa na vikwazo vya kiuchumi viliyochukuliwa na Marekani tangu mwaka 1979. Vikwazo vilizidishwa mwaka 2006 kufuatia mzozo wa nyuklia, huku uchumi wa Iran ukidorora mwaka 2012, wakati nchi za Ulaya zilijiunga na Marekani kwa kuichukulia vikwazo nchi hiyo.

Tangu mwaka 2012 uchumi wa Iran ulishuka hadi kupoteza dola bilioni 200.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.