Pata taarifa kuu
IRAN-NYUKLIA-USALAMA-DIPLOMASIA

Nyuklia ya Iran: mazungumzo ya kujaribu kukamilisha makubaliano

Mjini Vienna, mazungumzo juu ya nyuklia ya Iran yanaendelea licha ya kumalizika kwa tarehe ya mwisho hadi usiku wa manane wa Jumatatu Julai 13.

Wajumbe wa Iran na wale kutoka mataifa 5 + 1 yenye wakikutana kwa muda siku 17 kwa minajili ya mkataba.
Wajumbe wa Iran na wale kutoka mataifa 5 + 1 yenye wakikutana kwa muda siku 17 kwa minajili ya mkataba. REUTERS/Carlos Barria
Matangazo ya kibiashara

Mazungumzo kati ya mawaziri wa mambo ya nje wa Iran na mataifa 5 + 1 yenye nguvu yameendelea kwa kasi kwa muda wa wiki kadhaa. Kwani licha ya maendeleo, vikwazo vikubwa bado havijadiliwa.

Katika siku ya kumi na saba ya mazungumzo, mawaziri wote wa mambo ya nje walikuwepo katika mji wa Vienna, nchi Austria. Changamoto ni nyingi. Mkataba unapaswa kukamilishwa. Lakini kunatakiwa kwanza kujaribu kuondoa vikwazo, amekumbusha msemaji wa Ikulu ya Marekani, Josh Earnest.

" Hata katika wiki za hivi karibuni, kumekuwa na maendeleo makubwa. Baadhi pointi muhimu ya mazungumzo hayo zimepatiwa ufumbuzi, na hiyo ni dalili nzuri. Lakini bado zimesalia pointi muhimu ambazo hazijapatiwa ufumbuzi. Rais aliziomba timu zake kuendelea kushiriki katika mazungumzo na kushiriki kwa muda mrefu kama mazungumzo hayo yataendelea kuwa na manufaa. Kama wanaona ni muhimu kuendelea na mazungumzo haya na ni muhimu, timu ya mazungumzo itabaki katika mji wa Vienna ", amesema Josh Earnest.

Hatimaye, makubaliano hayo yangepelekea kuondolewa kwa vikwazo vya kimataifa dhidi ya Iran. Kanuni kuu ziliwekwa katika mji wa Lausanne mwezi Aprili. Tehran ilikubaliana kupunguza idadi ya vinu vya vya kuzalisha nyuklia pamoja na kiwango cha Uranium. Hizi ndizo taratibu.

Kila upande unataka kurudi na ushindi

Mazungumzo kati ya Tehran na mataifa 5 + 1 yenye nguvu yanaonekana kuendelea kwa kasi katika masaa ya hivi karibuni, amearifu mwandishi wa RFI katika mji wa Vienna, Sami Boukhelifa. Wengi miongoni mwa wanaoshiriki katika mazungumzo hayo mjini Vienna, wamesema si juu ya swala hili kwamba mazungumzo yatavunjika.

" Wataalam, wanasayansi wa kutoka mataifa yenye nguvu na Iran wamefanya vizuri kazi yao. Fani yao, ni sayansi halisi na matokeo yako wazi ", wamesema baadhi ya wajumbe hao katika mazungumzo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.