Pata taarifa kuu
IRAN-NYUKLIA-USALAMA-DIPLOMASIA

Mpango wa nyuklia wa Iran: mvutano waibuka Vienna

Katika mji mkuu wa Austria, Vienna, mazungumzo kuhusu mpango wa nyuklia wa Iran yameendelea kushika kasi. waziri wa mambo ya nje wa Ufaransa, Laurent Fabius, ameamua kufuta safari yake ya siku ya Jumatatu nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati na Ethiopia. Lakini hakuna matokeo ya uhakika ambayo yanaonekana kutoka katika mazungumzo hayo.

Katika usiku wa tarehe ya mwisho ya mazungumzo juu ya mpango wa nyuklia wa Iran Laurent Fabius amefuta safari zake mbili.
Katika usiku wa tarehe ya mwisho ya mazungumzo juu ya mpango wa nyuklia wa Iran Laurent Fabius amefuta safari zake mbili. REUTERS/Heinz-Peter Bader
Matangazo ya kibiashara

Kutokana na kukosekana kwa taarifa, mazungumzo juu ya mpango wa nyuklia wa Iran mjini Vienna yameanza kuibua uvumi kati ya raia mbalimbali zikiwemo nchi husika katika mazungumzo hayo. Jumapili, waziri wa mambo ya nje wa Ufaransa amekua na matumaini yenye tahadhari. "Natumaini hatimaye kuwa tumeingia katika awamu ya mwisho ya mazungumzo haya ya kasi (...) kwa kufikia matokeo yenye mafanikio", amesema Laurent Fabius.

Kwa mujibu wa mwandishi wa RFI, katika mji wa Vienna, Sami Boukhelifa, neno "kasi" halionekani kuwa na maana moja katika kila upande. Pande husika katika mazungumzo hayo haziafikiani kuhusu namna ya kudhibiti muda katika mazungumzo hayo. Nchi zenye nguvu duniani zinazoshiriki mazungumzo kuhusu mpango wa nyuklia wa Iran, hasa nchi za Magharibi, wanaharakia kuhitimisha mazungumzo. Iran, kwa upande wake, imethibitisha kuwa iko tayari kuendelea na mazungumzo katika muda utakaohitajika.

Matumaini, mashaka, yote hayo ni ishara tofauti zinazoonekana katika mji wa Vienna na matokeo bado hayajajulikana. Kwenye akaunti yake ya Twitter, mwanadiplomasia mmoja wa marekani amerusha mara tatu picha moja ya Rubik's Cube, anaetaka pengine kuonyesha jinsi gani kumekua na mvutano katika mazungumzo hayo. Msimamo wake huo unakinzana na ule wa mkuu wa sera za kidiplomasia wa Ulaya, Federica Mogherini, ambay amezungumzia kuwa hatua imefikia sasa ni ya maamuzi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.