Pata taarifa kuu
ISRAEL-PALESTINA-USALAMa

Israel: hali ya utulivu yarejea katika Msikiti wa Al-Aqsa

Maafisa wakuu wa usalama nchini Israel wamethibitisha kuwa kumekuwa na hali ya utulivu baada ya kushuhudiwa vurugu kubwa katika msikiti wa Al-Aqsa, Jerusalem Mashariki baada ya polisi wa Israel kuingia eneo la msikiti huo.

Askari polisi wa Israel wakiingia Jumapili katika Msikiti wa Al-Aqsa, Jerusalem, ambapo vurugu zilipotokea.
Askari polisi wa Israel wakiingia Jumapili katika Msikiti wa Al-Aqsa, Jerusalem, ambapo vurugu zilipotokea. REUTERS/Ammar Awad
Matangazo ya kibiashara

Eneo hilo limekuwa kiini cha mizozo ya kidini na kisiasa kati ya Israel na Wapalestina na hushuhudia makabiliano ya mara kwa mara.

Kwa mujibu wa gazeti la Jerusalem Post, Mashirika ya kutetea haki za binadamu yameshutumu polisi kutumia gesi ya kutoa machozi na guruneti za kudhibiti waandamanaji.

Al-Aqsa ni moja ya maeneo matakatifu zaidi miongoni mwa Waislamu, na msikiti huo unapatikana katika eneo la Haram al-Sharif ambalo pia ni takatifu kwa Wayahudi.

Mapigano hayo yametokea saa chache kabla ya kuanza kwa Mwaka Mpya wa Kiyahudi, Rosh Hashanah.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.