Pata taarifa kuu
SYRIA-IS-MAUAJI

Syria: IS yaimarisha makao makuu ya Deir Ezzor, hofu ya "mauaji"

Jumatano hii kundi la Islamic State (IS) limeimarisha ulinzi karibu na mji wa Deir Ezzor, mashariki mwa Syria, ambapo watu wanaishi katika hofu baada ya mauaji ya raia kadhaa na kutekwa nyara kwa wakazi wa mji huo zaidi ya mia moja.

mji wa Deir Ezzor en Syrie, Januari 4, 2016.
mji wa Deir Ezzor en Syrie, Januari 4, 2016. AFP/AHMAD ABOUD/AFP
Matangazo ya kibiashara

Mapambano makali yameendelea kwa siku ya tano mfululizo baada ya mashambulizi makubwa yalioanzishwa Jumamosi na kundi la IS katika mji wa Deir Ezzor, mji mkuu wa mkoa huo wenye utajiri wa mafuta, kilomita 450 kaskazini mwa mji wa Damascus.

Ndege za jeshi la Urusi, zikisaidia vikosi vya serikali ya Bashar Al Assad, zimeendesha mashambulizi ya anga dhidi ya mkoa wa Deir Ezzor, Wizara ya Ulinzi mjini Moscow imesema. Jeshi la Urusi pia limewapa tangu Januari 15 zaidi ya tani 50 ya misaada ya kibinadamu kwa wakazi wa mji huo.

Wanajihadi sasa wanadhibiti 60% ya mji, ambapo watu 200,000 bado wanaishi. Wamekua wakiimarisha ulinzi katika makao makuu kupitia maeneo ambayo bado mikononi mwa vikosi vya serikali katikati, magharibi na kusini-magharibi.

Kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa, karibu 70% ya wakazi wa maeneo yanayozingirwa ni wanawake na watoto.

"Watu wanaogopa, hali imekuwa ngumu zaidi", amesema Attiyeh, mkazi aliyehojiwa kwa njia ya simu. "Chakula na mboga ni ni nadra na tunaanza kuwa na matatizo na mkate."

IS hatimaye eneo la Al-Bgheliyeh, kitongoji cha kaskazini magharibi mwa mji, ambacho kilikua kituo kikuu cha kilimo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.