Pata taarifa kuu

Afghanistan: Marekani na Taliban zakabidhiana wafungwa

Marekani na utawala wa Taliban wamekabidhiana wafungwa kati ya mkongwe wa jeshi la wanamaji la Marekani na mfuasi mkuu wa vuguvugu la Kiislamu lililozuiliwa kwa miaka kumi na saba na Wamarekani, ametangaza Jumatatu Septemba 19, Waziri wa Mambo ya Nje wa Afghanistan.

Mmarekani Mark Frerichs, aliyetekwa nyara mwaka wa 2020 nchini Afghanistan, alibadilishwa na Bashar Noorzaï (katika ), mbabe wa kivita karibu na Taliban.
Mmarekani Mark Frerichs, aliyetekwa nyara mwaka wa 2020 nchini Afghanistan, alibadilishwa na Bashar Noorzaï (katika ), mbabe wa kivita karibu na Taliban. AFP - WAKIL KOHSAR
Matangazo ya kibiashara

Rais wa Marekani Joe Biden amethibitisha kuachiliwa kwa mhandisi wa Marekani Mark Frerichs kutoka mikononi mwa kundi la Taliban. "Mafanikio ya mazungumzo yaliyopelekea kuachiliwa kwa Mark yalihitaji maamuzi magumu, ambayo sikuyachukulia kirahisi," amesema rais huyo wa Marekani katika taarifa yake.

Mmarekani Mark Frerichs, aliotekwa nyara mwaka 2020 nchini Afghanistan, alibadilishwa na Bashar Noorzaï, mbabe wa kivita akishirikiana na Taliban aliyefungwa kwa miaka kumi na saba nchini Marekani kwa ulanguzi wa madawa ya kulevya aina ya heroin. "Baada ya mazungumzo marefu, raia wa Marekani Mark Frerichs alikabidhiwa kwa ujumbe wa Marekani na ujumbe huu kukabidhiwa kwetu (Bashar Noorzai) leo (Jumatatu) katika uwanja wa ndege wa Kabul," amesema waziri wa mambo ya nje wa Afghanistan, Amir Khan Muttaqi, katika mkutano na vyomo vya habari. mkutano uliofanyika katika mji mkuu.

Mkongwe huyo wa Jeshi la Wanamaji la Marekani alikuwa akifanya kazi kama mhandisi wa ujenzi katika miradi ya ujenzi nchini Afghanistan alipotekwa nyara na watu hao, kulingana na Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani. Bashar Noorzai, aliyehukumiwa kifungo cha maisha jela nchini Marekani kwa ulanguzi wa madawa ya kulevya aina ya heroin, hakuwa na cheo rasmi ndani ya kundi la Taliban, msemaji wa serikali ya Afghanistan Zabihullah Mujahid ameliambia shirika la habari la AFP. Hata hivyo "alitoa msaada mkubwa, ikiwa ni pamoja na silaha", wakati wa lililpobuka vuguvugu la Kiislamu katika miaka ya 1990, ameongeza.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.