Pata taarifa kuu

Afghanistan : Marekani yakutana na uongozi wa Taliban nchini Qatar

Marekani inatoa wito kwa uongozi wa Taliban nchini Afghanistan, kubadilisha será zake, zinazokwenda kinyume cha haki za binadamu hasa dhidi ya wanawake na wasichana nchini humo.

Marekani imewataka viongozi wa Taliban kuwaruhusu wasichana kwenda Shuleni na kuwaruhusu wanawake kuajiriwa. 
Marekani imewataka viongozi wa Taliban kuwaruhusu wasichana kwenda Shuleni na kuwaruhusu wanawake kuajiriwa.  AP - Rodrigo Abd
Matangazo ya kibiashara

Wito huu umetolewa na Marekani, nchini Qatar wakati wa mazungumzo ya Kwanza kati yake na viongozi wa Taliban yaliyofanyika kwa siku mbili zilizopita. 

Marekani imewataka viongozi wa Taliban kuwaruhusu wasichana kwenda Shuleni na kuwaruhusu wanawake kuajiriwa. 

Aidha, Washington inataka kuachiwa kwa raia wake, wanaoendelea kushikiliwa na uongozi wa Taliban. 

Kwa upande wa Taliban, wanaitaka Marekani kuondoa vikwazo vya kusafiri, vilivyowekewa viongozi wake. 

Tangu mwezi Agosti mwaka 2021 kundi hilo limekuwa likiongoza nchini Afganistan baada ya kuondoka kwa wanajeshi wa Marekani. 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.