Pata taarifa kuu

Kesi dhidi ya Israel kwenye Mahakama ya Kimataifa ya Haki, ICJ yaanza

Mahakama ya Kimataifa ya Haki ICJ, imeanza kusikiliza kesi iliyowasilishwa na Afrika Kusini, ikiituhumu Israeli kutekeleza mauaji ya kimbari kufuatia operesheni yake dhidi ya kundi la Hamas kwenye ukanda wa Gaza, tangu Oktoba 7 mwaka uliopita. 

Mahakama ya Kimataifa ya Haki jijini Hague, Januari 11 2024
Mahakama ya Kimataifa ya Haki jijini Hague, Januari 11 2024 REUTERS - THILO SCHMUELGEN
Matangazo ya kibiashara

Wakati kesi hiyo ikianza jijini Hague, nje ya Mahakama, kulikuwa na waandamanaji kutoka Palestina na Israel, huku polisi wakiwa katikati yao kuzuia makabiliano. 

 

Mawakili kutoka Afrika Kusini, wanataka Mahakama hiyo iagize Israeli isitishe operesheni za kijeshi kwenye ukanda wa Gaza. Wanasisitiza kuwa shambulio la Hamas halipaswi kutumiwa kama sababu na Israeli kuhalalisha vitendo vyake dhidi ya Wapalestina. 

 

Wapalestina wamevumilia oparesheni za mara kwa mara na ghasia kwa miaka 76 zilizopita. Hakuna shambulio la silaha dhidi ya ardhi ya nchi, hata liwe kubwa kiasi gani,” amesema Ronald Lamola, waziri wa masuala ya haki wa Afrika Kusini. 

Waandamanaji wa Israeli wakiwa nje ya Mahakama ya ICJ jijini Hague, Januari 11 2024
Waandamanaji wa Israeli wakiwa nje ya Mahakama ya ICJ jijini Hague, Januari 11 2024 AFP - ROBIN UTRECHT

Mahakama hiyo ya ICJ, inatarajiwa kutoa uamuzi wa maoni iwapo mashtaka dhidi ya Israeli kuwa inatekeleza mauaji ya kimbari ni sahihi kwa sababu, kesi iliyo mbele yake sio ya jinai.  Hii ilikuwa kauli ya rais wa mahakama  hiyo Joan Donoghu wakati wa ufunguzi wa kesi hiyo. 

 

“Afrika Kusini inasisitiza kuwa vitendo vya Israel, ambavyo inalalamikia, ni vya kimbari, kwa sababu, na nukuu, “zimekusudiwa kuleta uharibifu wa sehemu kubwa ya kundi la Wapalestina, ikiwemo kundi la Wapalestina katikaukanda wa Gaza,” amesema

  

 Israeli imekanusha madai kuwa inatekeleza mauaji ya kimbari, huku  ikitarajiwa kutoa utetezi wake siku ya Ijumaa wakati huu jeshi lake likiendeleza mashambulio kwenye ukanda wa Gaza na kuongeza idadi ya vifo ambavyo vimevuka Elfu 23. 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.