Saudi Arabia yatoa wito kwa Israel 'kuwajibikia' kwa 'ukiukaji' wa sheria za kimataifa
Saudi Arabia siku ya Ijumaa imekaribisha uamuzi wa Mahakama ya Kimataifa ya Haki (ICJ) kuhusu Israel, ikitoa wito kwa jumuiya ya kimataifa "kuiwajibisha Israel" kwa "ukiukaji wake" wa sheria za kimataifa.
Imechapishwa:
Katika taarifa kutoka Wizara ya Mambo ya Nje, Saudi Arabia pia imetoa wito wa "hatua zaidi" kufikia "kusitishwa kwa mapigano katika Ukanda wa Gaza" na kutoa "ulinzi kwa raia wa Palestina".
Katika uamuzi uliotarajiwa sana, mahakama ya juu zaidi ya Umoja wa Mataifa imetoa wito siku ya Ijumaa Januari 26 kwa Israel kufanya kila linalowezekana kuzuia kitendo chochote cha "mauaji ya kimbari" katika Ukanda wa Gaza na kuruhusu misaada ya kibinadamu kuingia.
Katika hatua hii ya kesi, ICJ pia haijatoa uamuzi wazi juu ya suala la madai ya mauaji ya kimbari ya Israel huko Gaza. Lakini hata hivyo inaona kuwa ni vitendo kama hivyo vinaweza kufanywa, anabaini mwandishi wetu huko The Hague, Stéphanie Maupas.