Pata taarifa kuu

ICJ yaitaka Israel kuzuia vitendo vya 'mauaji ya halaiki' Gaza

Israel inapaswa kuzuia kitendo chochote kinachowezekana kusababisha mauaji ya halaiki na kuruhusu upatikanaji wa misaada ya kibinadamu Gaza: hivi ndivyo Mahakama ya Kimataifa ya Haki imeamua siku ya Ijumaa, Januari 26, katika hukumu iliyotarajiwa sana, ambayo hata hivyo haikutaja kusitishwa kwa mapigano katika Ukanda wa Gaza.

(Kushoto kwenda kulia) Waziri wa Mambo ya Nje wa Afrika Kusini, Naledi Pandor, pamoja na Mshauri wa Kisheria wa Rais wa Afrika Kusini, Nokukhanya Jele na Balozi wa Afrika Kusini nchini Uholanzi, Vusimuzi Madonsela, baada ya uamuzi uliotolewa na Mahakama ya Kimataifa ya Haki kuhusu Israel, mjini Hague, Uholanzi, Januari 26, 2024.
(Kushoto kwenda kulia) Waziri wa Mambo ya Nje wa Afrika Kusini, Naledi Pandor, pamoja na Mshauri wa Kisheria wa Rais wa Afrika Kusini, Nokukhanya Jele na Balozi wa Afrika Kusini nchini Uholanzi, Vusimuzi Madonsela, baada ya uamuzi uliotolewa na Mahakama ya Kimataifa ya Haki kuhusu Israel, mjini Hague, Uholanzi, Januari 26, 2024. © PIROSCHKA VAN DE WOUW / Reuters
Matangazo ya kibiashara

 

Mahakama ya Kimataifa ya Haki (ICJ) imeamua: Israel lazima ifanye kila iwezalo "kuzuia" kitendo chochote cha "mauaji ya kimbari" katika Ukanda wa Gaza, na hakuna kiongozi anayepaswa kutoa matamshi ya kuchochea mauaji ya halaiki, mahakama imetangaza katika makao yake huko Hague, Uhispania. Kwa kuongeza, "Israel inapaswa kuchukuwa hatua madhubuti mara moja ili kuwezesha utoaji wa huduma za kimsingi na misaada ya kibinadamu," ICJ imeongeza katika uamuzi wake, uliofuatwa duniani kote. Mahakama imetaja "hali mbaya ya kibinadamu" huko Gaza "inaweza kusababisha hatari kubwa ya kuzorota zaidi kwa usalama" na kusababisha uharibifu usioweza kurekebishwa katika eneo hilo.

Majaji wameitaka Israel isifanye mauaji, isizuie kuzaliwa kwa watoto huko Gaza, isifanye maisha ya Wapalestina kutowezekana, na isisababishe mashambulizi dhidi ya uadilifu wao wa kiakili na kimwili. Kwa sababu vitendo hivi vyote vinaweza kuwa mauaji ya halaiki ikiwa vitafanywa kwa nia ya kuwaangamiza Wapalestina huko Gaza.

Kwa kutoa uamuzi wake, ICJ imezingatia kwamba haikuwa na uthibitisho wa idadi ya wahanga huko Gaza, lakini ilijikita kwenye ripoti rasmi kutoka Umoja wa Mataifa, ambayo inasema karibu wakazi wote wa Gaza watapata madhara ya kimwili au ya kisaikolojia kutokana na operesheni za kijeshi zinazoendeleaa, anaripoti mwandishi wetu wa Brussels, Pierre Benazet. Asilimia 93 ya watu wa Gaza wanakabiliwa na njaa kwa viwango tofauti na watu milioni 1.7 wamelazimika kuyahama makazi yao kutokana na mzozo huo.

Hakuna wito wa kusitisha mapigano

Kwa upande mwingine, hatua tatu kati ya zilizoombwa hazikutolewa. Kwa mfano, Mahakama haikuamuru kusimamishwa kwa operesheni za kijeshi za Israeli, kama ilivyoombwa na Afrika Kusini, kwa asili ya utaratibu uliozinduliwa mwezi wa Desemba mwaka uliyopita. Nchi hiyo ilipeleka suala hilo mahakamani, ikiamini kuwa Israel inakiuka Mkataba wa Umoja wa Mataifa wa Mauaji ya Kimbari ya mwaka 1948.

Katika hatua hii ya kesi, ICJ pia haijatoa uamuzi wazi juu ya suala la madai ya mauaji ya kimbari ya Israel huko Gaza. Lakini hata hivyo inaona kuwa ni vitendo kama hivyo vinaweza kufanywa, anabaini mwandishi wetu huko Hague, Stéphanie Maupas.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.