Pata taarifa kuu

Israeli: Shule zafungwa kwa sababu za usalama

Jeshi la Israel limetangaza siku ya Jumamosi, Aprili 13, 2024, kufungwa kwa shule kwa sababu za kiusalama baada ya vitisho vya Iran kujibu shambulio baya lililotekelezwa mwanzoni mwa mwezi Aprili dhidi ya ubalozi mdogo wa Iran mjini Damascus, unaohusishwa na Israel.

Msemaji wa jeshi ametoa wito kwa raia kuwa "macho na kuwajibika". "Mifumo ya ulinzi na mashambulizi ya Jeshi la Anga iko macho na ndege nyingi zinashika doria angani, zimejiandaa na ziko tayari (...) Tuna mfumo bora wa ulinzi wa anga, lakini ulinzi haupitiki hewani," ameongeza.
Msemaji wa jeshi ametoa wito kwa raia kuwa "macho na kuwajibika". "Mifumo ya ulinzi na mashambulizi ya Jeshi la Anga iko macho na ndege nyingi zinashika doria angani, zimejiandaa na ziko tayari (...) Tuna mfumo bora wa ulinzi wa anga, lakini ulinzi haupitiki hewani," ameongeza. REUTERS/Nir Elias
Matangazo ya kibiashara

Kuanzia Jumapili, siku ya kwanza ya juma nchini Israeli, "shughuli za kufundisha, safari na matembezi" shule au masomo ya ziada yamesimamishwa, msemaji wa jeshi Daniel Hagari amesema katika hotuba ya video.

Hatua iliyoamuliwa "kuhusu hali ya usalama" ni halali katika hatua hii kwa siku mbili, Jumapili na Jumatatu. Kama sehemu ya vikwazo hivi, mapokezi na safari za kituo cha burudani pia zimefutwa. Pessah, Pasaka ya Kiyahudi, inapokaribia, mikusanyiko ya nje itapunguzwa idadi ya watu na kuwa na watu 1,000 na idadi itakayozuiliwa zaidi katika maeneo ya mpaka wa nchi, ambapo fukwe zitafungwa.

Shughuli za kitaaluma haziathiriwa na hatua hii. Msemaji wa jeshi ametoa wito kwa raia kuwa "macho na kuwajibika". "Mifumo ya ulinzi na mashambulizi ya Jeshi la Anga iko macho na ndege nyingi zinashika doria angani, zimejiandaa na ziko tayari (...) Tuna mfumo bora wa ulinzi wa anga, lakini ulinzi haupitiki hewani," ameongeza.

Waziri wa mambo ya nje wa Israel, Israel Katz, kwa upande wake, amebaini kwamba amefuta safari iliyopangwa nchini Austria na Hungary pamoja na familia za mateka wanaozuiliwa huko Gaza. Iran imeapa kulipiza kisasi baada ya shambulio mbaya la Aprili 1 dhidi ya ubalozi wake mdogo huko Damascus, operesheni ambayo inalaumu Israeli. Rais wa Marekani Joe Biden alisema siku ya Ijumaa alitarajia Iran itachukua hatua "hivi karibuni" na kuionya kujizuia.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.