Pata taarifa kuu

Meli iliyokamatwa na Iran: Israel yaitaka EU kuainisha Walinzi wa Mapinduzi kama 'kundi la kigaidi'

Waziri wa Mambo ya Nje wa Israel, Israel Katz, ametoa wito kwa Umoja wa Ulaya (EU) kuweka kwenye orodha ya "makundi ya kigaidi" Walinzi wa Mapinduzi ya Iran, jeshi la kiitikadi la Jamhuri ya Kiislamu, ambalo limeteka Jumamosi Aprili 13, meli ya mizigo katika Ghuba.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Israel, Israel Katz wakati wa mkutano wa kila wiki wa baraza la mawaziri huko Jerusalem mnamo Februari 24, 2019.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Israel, Israel Katz wakati wa mkutano wa kila wiki wa baraza la mawaziri huko Jerusalem mnamo Februari 24, 2019. Abir Sultan/Pool via REUTERS
Matangazo ya kibiashara

"Ninatoa wito kwa Umoja wa Ulaya na ulimwengu huru kutangaza mara moja Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Irani kama kundi la kigaidi na kuiwekea vikwazo Iran mara moja," ameandika Israel Katz kwenye mtandaowa X (zamani ikiitwa Twitter), akishutumu "utawala wa uhalifu" nchini Iran.

Meli hiyo iitwayo 'MCS Aries' inamilikiwa na bilionea wa Israel. Ilikamatwa na Jeshi la Wanamaji la Walinzi wa Mapinduzi la Sepah. Meli hiyo ilielekezwa kwenye maji ya eneo la Irani.

Kwa mujibu wa baadhi ya tovuti zilizobobea, hii ni sehemu ya jibu la Tehran kwa shambulio la ubalozi mdogo wa Aprili 1, ambalo lilisababisha vifo vya watu kumi na sita, wakiwemo maafisa wawili wa ngazi za juu wa kikosi maalumu cha Walinzi wa Mapinduzi. Hii inaonyesha kuwa Tehran iko tayari kwa hali yoyote itakayotokea.

Wakati huo huo, Iran inaonya kwamba ikiwa serikali ya Israel itachukua hatua, kutakuwa na jibu kali zaidi kutoka kwa Iran na matarajio ya mzozo huo kuongezeka katika eneo lote.

Katika siku za hivi karibuni, washirika wa Tehran katika ukanda huo, hususan Hezbollah ya Lebanon, Houthis nchini Yemen na wanamgambo wa Kishia wa Iraq, wameongeza mashambulizi dhidi ya Israel.

Tehran imeionya Washington dhidi ya uwezekano wowote wa kuiunga mkono Israel katika tukio la shambulio la Iran. Kambi za Marekani zinaweza kulengwa na Tehran na washirika wake.

Wafanyakazi 25 wako kwenye meli iliyokamatwa Jumamosi hii, amesema mmiliki wa meli hiyo ya MSC, raia mwenye uraia pacha Italia na Uswisi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.