Pata taarifa kuu

Wafaransa watahadharishwa kusafiri kwenda Iran, Israel, Lebanon na maeneo ya Palestina

Ufaransa imewataka raia wake "kujizuia kabisa"  kusafiri katika siku zijazo kwenda Iran, Lebanon, Israel na maeneo ya Palestina "inayokabiliwa na hatari ya kuongezeka kwa mashambulizi", baada ya vitisho vya Tehran kuapa kulipiza kisasi dhidi ya Israel.

Stéphane Séjourné, Waziri wa Mambo ya Nje wa Ufaransa.
Stéphane Séjourné, Waziri wa Mambo ya Nje wa Ufaransa. © RFI/France 24
Matangazo ya kibiashara

Mkuu wa diplomasia ya Ufaransa Stéphane Séjourné "anawataka Wafaransa kujizuia kabisa kusafiri katika siku zijazo kwenda Iran, Lebanon, Israel na maeneo ya Palestina," wasaidizi wake wameliambia shirika la habari la AFP siku ya Ijumaa.

Uamuzi huo unakuja wakati Iran ikitishia kuishambulia Israel, inayoshutumiwa kwa shambulio la Aprili 1 kwenye ubalozi mdogo wa Iran huko Damascus, nchini Syria, na "ilizingatiwa katika mkutano wa mgogoro", anabainisha waziri wa Mambo ya Nje wa Ufaransa. Pia ametoa wito wa "kurejeshwa kwa familia za maafisa wa kidiplomasia kutoka Tehran" pamoja na marufuku kwa misheni za maafisa wa Ufaransa katika nchi hizi.

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ali Khamenei ameapa "kuiadhibu" Israel kwa kujibu mauaji ya wanajeshi saba wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi katika shambulio linalohusishwa Israel dhidi ya ubalozi mdogo wa Iran mjini Damascus tarehe 1 Aprili. Serikali ya Israel inasema iko tayari kujiandaa kwa hali yoyote na inatishia Iran kwa kulipiza kisasi iwapo kutatokea shambulio katika ardhi yake.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.