Pata taarifa kuu

Wakuu wa diplomasia wa G7 watoa wito wa 'kuzuia kuongezeka kwa uhasama'

“Kwa kuzingatia mashambulizi ya Aprili 19, tunatoa wito kwa pande zote kufanya kazi ili kuzuia kuongezeka kwa uhasama. G7 itaendelea kufanya kazi katika mwelekeo huu,” wamesema mawaziri wa mambo ya nje wa nchi za G7 (Marekani, Japan, Ujerumani, Canada, Ufaransa, Uingereza na Italia) siku ya Ijumaa katika taarifa ya mwisho iliyochapishwa mwishoni mwa mkutano wao.

Shirika la habari la FARS limeripoti milipuko mitatu karibu na kambi ya kijeshi huko Qahjavarestan, kati ya mji wa Isfahan na uwanja wake wa ndege, katikati mwa nchi.
Shirika la habari la FARS limeripoti milipuko mitatu karibu na kambi ya kijeshi huko Qahjavarestan, kati ya mji wa Isfahan na uwanja wake wa ndege, katikati mwa nchi. © Studio graphique FMM
Matangazo ya kibiashara

Waziri wa Mambo ya Nje wa Italia Antonio Tajani, ambaye nchi yake ni mwenyekiti wa G7 mwaka huu, amefafanua wakati wa mkutano na waandishi wa habari kwamba ajenda ya kazi ya Ijumaa asubuhi ilibadilishwa ili kujumuisha milipuko nchini Iran. "G7 inajitahidi kufikia usitishwaji wa uhasama," amesisitiza, akibainisha kuwa "Marekani ilifahamishwa dakika za mwisho" kuhusu mashambulizi haya. Iran "imefungua tena anga yake," ameongeza.

Moscow yatoa wito kwa pande zinazokinzana "kujizuia"

Ikulu ya Kremlin siku ya Ijumaa imetoa wito kwa pande zote zinazkinzana "kujizuia" ili kuepusha "kuongezeka kwa uhasama", kujibu habari zinazohusiana na milipuko nchini Iran inayohusishwa na baadhi na Israeli, hata hivyo Moscow imejiepusha kutaja mhusika wa mashambulizi hayo.

"Tunaendelea kuhimiza wahusika kujizuia na kujiepusha na hatua zozote zinazoweza kusababisha ongezeko jipya la uhasama katika eneo nyeti kama hilo," msemaji wa Kremlin Dmitri Peskov amesema, akisema kwamba ni "mapema sana" kutoa maoni juu ya dhima yoyote inayowezekana, katika kutokuwepo kwa taarifa rasmi kutoka Israel.

Iran yadai "kuharibu" "kitu kilichotiliwa shaka"

"Ripoti za vyombo vya habari vya Marekani si sahihi," msemaji wa shirika la anga za juu la Iran Hossein Dalirian amesema. Amesema "hakujawa, hadi sasa, mashambulizi yoyote ya anga kutoka nje ya mipaka dhidi ya Isfahan au maeneo mengine ya nchi."

"Walifanya tu jaribio lililoshindwa na la kufedhehesha kwa kurusha kifaa kinachofanana na droni, ambayo imedunguliwa," ameongeza katika ujumbe uliotumwa kwenye mtandao wa X, bila kutoa maelezo juu ya waliohusika na vitendo hivi.

Kwa mujibu wa Gazeti la Marekani la The New York Times, ambalo limenukuu maafisa wa Iran, shambulio hilo lilifanywa na ndege ndogo zisizo na rubani, ambazo huenda zilirushwa kutoka ardhi ya Iran, na ulinzi wa anga "haukugundua vitu visivyojulikana vinavyoruka kwenye anga ya Iran.

"Mlipuko wa leo katika anga ya Isfahan ulihusishwa na kurusha mifumo ya ulinzi ya ndege kwenye kitu cha kutiliwa shaka ambacho hakikusababisha ajali yoyote au uharibifu," amesema Kamanda Mkuu wa jeshi, Abdolrahim Mousavi, kulingana na shirika la habari la Tasnim.

"Wataalamu wanachunguza ukubwa wa tatizo na watatoa taarifa baada ya kupokea matokeo," ameongeza. "Tayari mumeona majibu ya Iran," kamanda amesema juu ya jibu linalowezekana lililoamuliwa na Tehran.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.