Pata taarifa kuu
UHISPANIA-UEFA

Barcelona yaiondoa Manchester City katika kinyanganyiro cha UEFA

Klabu ya Barcelona imejikatia tiketi jana jumatano ya kuingia katika robo fainali katika michuano ya klabu bingwa barani Ulaya, baada ya kuimenya nyumbani Manchester City kwa mabao 2-1. Katika kipindi cha kwanza cha mchezo, timu hizo mbili zilienda sare ya kutofungana. Mabaao ya Barça yamewekwa kimyani na Messi katika dakika ya 67, pamoja na Dani Alves katika dakika ya kwanza ya majeruhi, baada ya dakika 90 kumalizika.

Wachezaji wa Barcelona wakifurahia ushindi
Wachezaji wa Barcelona wakifurahia ushindi REUTERS
Matangazo ya kibiashara

Barcelona imepata ushindi huo, baada ya kuwachezesha katika mchuano wa jana wachezaji nyota, ambao ni Xavi, Andres Iniesta, Cesc Fabregas pamoja na Lionel Messi.

Mshabuliaji na akiwa mfungaji katika mchuano wa jana, mchezaji wa Manchester City, Sergio Agüero, amepata jeraha la mguu, na aliondolea kabala kumalizika kwa mchuaon huo, na bado haijaaminika iwapo atacheza katika mchuano wa jumamosi dhidi ya Hull katika michuano ya ligi kuu ya Wingereza ambayo inaendelea.

“Bado ni mapema kusema kwamba Sergio Agüero, hatocheza mchuano wa jumamosi, lakini jeraha alilopata si kubwa”, amesema kocha msaidizi wa Machester City Ruben Cousillas.

Manchester City imejaribu kumtumia James Milner ili asaidizane na Samir Nasri pamoja na David Silva, huku Sergio Agüero akisalia katikati bila mafanikio.

Wachezaji wa klabu ya FC Barcelone waliyocheza katika mchuano wa jana ni pamoja na Valdes, Dani Alves, Piqué, Mascherano, Jordi Alba, Xavi, Sergio Busquets, Iniesta - Fabregas, Messi, Neymar.

Huku Manchester City ikiwa na wachezaji wafuatao : Hart , Zabaleta, Kompany, Lescott, Kolarov, Fernandinho, Touré, Milner, Silva, Nasri, Agüero.

 

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.