Pata taarifa kuu

Michuano ya robo fainali ya kuwania taji la klabu bingwa Ulaya.

Real Madrid ya Uhispania watakuwa nyumbani kumenyana na Borrusia Dortmund ya Ujerumani, huku Paris Saint-Germain ya Ufaransa ikimenyana na Chelsea ya Uingereza.

Wachezaji wa klabu ya  Borussia Dortmund wakiwa katika mazoezi katika uwanja wa Santiago Bernabeu stadium mjini Madrid
Wachezaji wa klabu ya Borussia Dortmund wakiwa katika mazoezi katika uwanja wa Santiago Bernabeu stadium mjini Madrid REUTERS/Susana Vera
Matangazo ya kibiashara

Real Madrid na Borrusia Dortmund wanakutana tena baada ya kuchuana katika hatua ya nusu fainali mwaka uliopita, mchuano ambao Borrusia Dortmund walipata ushindi.

Madrid ambao wameshinda taji hilo mara tisa wapo katika hatua ya robo fainali mara nne mfululizo na vijana wa Kocha Cralo Ancelloti wanatarajia kutumia uwanja wao wa nyumbani wa Santiago Bernabéu kupata ushindi mkubwa kabla ya mchuano wa marudiano tarehe nane mwezi huu.

Kocha wa Chelsea Jose Mourhino naye atakuwa ugenini kujaribu kupata ushindi ambao utamsaidia kusonga mbele na kushinda taji hilo akiwa na klabu tofauti.

Siku ya Jumanne usiku michuano mingine ya robo fainali ilichezwa katika viwanja mbalimbali barani Ulaya.

Barcelona ya Uhispania wakiwa nyumbani walitoka sare ya bao 1 kwa 1 dhidi ya watani wao Atletico Madrid pia ya Uhispania.

Bao la Barcelona lilitiwa kimyani na Neymar De Silva Santos katika dakika ya 72 ya mnchuano huo, huku bao la Atletico Madrid likipatikana mapema katika dakika ya Diego Ribas da Cunha katika dakika 56 ya mchuano huo.

Mchuano mwingine kati ya Manchster United na FC Bayern Munich ya Ujerumani pia ulimalizika kwa sare ya bao 1 kwa 1 katika uwanja wa Old Trafford nchini Uingereza.

Michuano ya marudiano itachezwa baada ya wiki moja kutafuta timu zitakazofuzu katika hatua ya nusu fainali.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.