Pata taarifa kuu
Ghana

Chama cha soka nchini Ghana chakanusha tuhma za kupanga matokeo

Rais wa chama cha soka nchini Ghana amekanusha madai kuwa chama hicho kilikubali timu ya Taifa 'The Black Stars” kucheza mechi ambazo mataifa mengine yalikuwa yamejiandaa kupanga matokeo yake.

Kikosi cha timu ya taifa ya Ghana
Kikosi cha timu ya taifa ya Ghana fifa.com
Matangazo ya kibiashara

Tuhma hizo zimechapishwa na Gazeti la Uingereza la The Daily Telegraph na rais wa chama hicho Kwesi Nyantakyi amenukuliwa akisema sio kweli.

Nyantakyi anataka polisi nchini Uingereza kuchunguza madai ya Gazeti hilo na kituo cha runinga cha Channel 4 ambazo zimekuwa zikichunguza tuhma hizo dhidi ya wawakilishi hao wa Afrika huko Brazil.

Uchunguzi wa vyombo hivyo vya habari unaeleza kuwa watu wawili, wanaofahamika , mmoja akiwa wakala wa FIFA na mwingine kutoka chama cha soka cha Ghana, walikuwa wamepanga matokeo ya timu ya Ghana na timu ambazo hazikutajwa baada ya michuano ya kombe la dunia.

Shirikisho la soka duniani FIFA linasema halijapata ushahidi wowote kuwa michuano ya kombe la dunia inayoendelea imeingiliwa na matokeo yanapangwa.

Hata hivyo, FIFA inaonya kuwa itamwekea vikwazo yeyote atakayebainika kuhusika kwa namna moja au nyingine na upagaji wa matokeo katika michuano ya kombe la dunia.

Ghana ambayo inashiriki kombe la dunia, imetoka sare ya mabao 2 kwa 2 na Ujerumani na kufungwa mabao 2 kwa 1 na Marekani na itacheza na Ureno tarehe 26 mwezi huu kuamua hatima yake katika michuano hii.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.