Pata taarifa kuu
MOROCCO-MICHUANO YA RIADHA

Morocco yajiandaa kupokea michuano ya riadha 2014

Morocco moja kati ya mataifa ya Afrika inajiandaa kupokea michuano ya riadha itakayowashirikisha wanariadha bora kutoka mataifa ya Afrika, michuano ambayo itachezwa kuanzia Ogasti 10 hadi 14 katika mji wa Marrakech.

Abdelaati Iguider
Abdelaati Iguider AFP PHOTO / GABRIEL BOUYS
Matangazo ya kibiashara

Wanariadha kutoka Morocco wanajianda kwa kushiriki michuano hiyo, baada ya miaka kadhaa kushindwa kufanya vizuri. Hata katika michuano ya riadha ya kimataifa na michezo ya Olimpiki, Morroco haijafanya vizuri.

Morocco ni moja ya nchi za Afrika ambazo zinapongezwa kwa maandalizi ya michezo ya kimataifa. Mji wa Marrakech unajiandaa kupokea michezo mbalimbali, hususan michuano ya riadha itakayowashirikisha wanariadha kutoka mataifa ya Afrika ( kuanzia Ogasti 10 hadi 14), michuano ya kombe la jumuiya ya madola barani Afrika (Septemba 13 hadi14), michuano ya kombe la dunia la klabu bingwa (Desemba 10 hadi 20) na baadae michuano ya kombe la mataifa ya Afrika (Januari 17 hadi Februari 8 mwaka 2015).

Morocco ni nchi ya nne barani Afrika ambayo ilikua ikifanya vizuri katika michezo ya riadha, baada ya kutwaa medali 19 mkiwemo 6 za dhahabu

Kwa leo, Morocco inakabiliwa na changa moto nyingi katika riadha, baada ya Hicham El Guerrouj kustaafu, miaka 10 iliyopita. Guerrouj alipeperiusha bendera ya Morocco mwaka 2004 baada ya kufanya vizuri kwenye umbali wa mita 1 500 na 5 000, wanariadha wengine waliofuata ni Nawal El Moutawakel, Khalid Skah, Jaouad Gharib au hata Nezha Bidouane Lakini kwa sasa Abdelaati Iguider peke yake ndiye anaeongoza nchinbi Morocco.

Jina la Iguider, mshindi wa michezo ya riadha mwaka 2012 aliyeshindana kwenye umbali wa mita 1 500 litawekwa mwanzo kwenye orodha ya wanariadha watakaoshiriki michuano hiyo ya riadha nchini Morocco, michuano itakayochezwa kuanzia Ogasti 10 hadi 14 mwaka 2014.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.