Pata taarifa kuu
SOKA-MICHUANO YA KLABU BINGWA UEFA

Soka: Manchester City yaburuzwa ikiwa nyumbani

Machester city wakiwa nyumbani wamefungwa na CSKA Moscow ya Urusi kwa mabao 2 kwa 1 huku Chelsea wakitoka sare ya bao 1 kwa 1 na Maribor.

wachezaji wa klabu ya wasan Manchester City, wakipigwa na mshangao baada ya kukanyagwa na CSKA Moscow ya Urusi kwa mabao 2 kwa 1, Jumatano Novemba 5 mwaka 2014.
wachezaji wa klabu ya wasan Manchester City, wakipigwa na mshangao baada ya kukanyagwa na CSKA Moscow ya Urusi kwa mabao 2 kwa 1, Jumatano Novemba 5 mwaka 2014. REUTERS/Darren Staples
Matangazo ya kibiashara

Katika matokeo ya michuano ya klabu bingwa barani Ulaya, vilabu kutoka nchini Uingereza vimeshindwa kufanya vizuri kinyume na matarajio ya wengi.

Meneja wa klabu ya Manchester City, Roberto Mancini akipigwa na bumbuwazi baada ya klabu yake kumenywa ikiwa nyumbani.
Meneja wa klabu ya Manchester City, Roberto Mancini akipigwa na bumbuwazi baada ya klabu yake kumenywa ikiwa nyumbani. REUTERS/Darren Staples

Katika mchuano wa Manchseter city, wachezaji Fernandinho na Yaya Toure walioneshwa kadi nyekundu baada ya kukosa nidhamu uwanjani na watakosa mchuano ujao dhidi ya Bayern Munich.

Bayern Munich wamewashinda Roma ya Italia kwa mabao 2 kwa 0, huku Paris Saint Germain ikipata ushindi mwembaba wa mbao 1 kwa 0 dhidi ya Apoel FC ya Cyprus.

Paris Saint-Germain, Barcelona, Porto na Bayern Munch zimefuzu katika hatua ya kumi na sita bora.

Hayo yakijiri mshambuliaji wa kimataifa wa timu ya taifa ya soka ya Argetina na klabu ya Barcelona nchini Uhispania, Lionel Messi amefikia rekodi iliyowekwa na mchezaji wa zamani wa klabu ya Real Madrid Raul kwa kufunga mabao 71 katika michuano hii ya klabu bingwa barani Ulaya.

Messi alifikia idadi hiyo Jumatano Novemba 5 usiku baada ya kufunga mabao 2 wakati klabu yake ikicheza na klabu ya Ajax katika michuano hii ya klabu bingwa huko Ulaya.

Lionel Messi amemfikia Raul baada ya mechi 90 ya UEFA, ikilinganiswa na Raul aliyefunga mabao hayo baada ya mechi 142.

Kwa sasa, Messi anafatwa na kwa karibu na mshambuluaji wa Real Madrid Christiano Ronaldo ambaye ana mabao 70 baada ya mechi 107 ya UEFA.

Ushindi wa Jumatano Novemba 5 umeisaidia Barcelona kufuzu katika hatua ya kumi na sita bora.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.