Pata taarifa kuu
TANZANIA-CAF-SOKA

TFF : Boniface Mkwasa kocha wa muda wa Taifa Stars

Shirikisho la soka nchini Tanzania TFF limemteua Boniface Mkwasa kuwa kocha wa muda wa timu ya taifa ya soka Taifa Stars. Tangazo hili limetolewa na rais wa TFF Jamal Malinzi jijini Dar es salaam Jumanne wiki hii.

Dutchman Mart Nooij, aliye kuwa kocha wa timu ya soka ya taifa ya Tanzania ( Taifa Stars).
Dutchman Mart Nooij, aliye kuwa kocha wa timu ya soka ya taifa ya Tanzania ( Taifa Stars).
Matangazo ya kibiashara

Mkwasa ambaye pia ni kocha msaidizi wa klabu ya Yanga anaanza kazi mara moja kuiandaa taifa Stars katika mchuano wa marudiano wa kuwania kufuzu katika fainali za CHAN kwa wachezaji wanaocheza soka nyumbani dhidi ya Uganda mapema mwezi ujao jijini Kampala.

Mkwasa anachukua mikoba ya Mholanzi Mart Nooij aliyefutwa kazi baada ya matokeo mabaya katika michuano kadhaa ya Kimataifa hususan baada ya kufungwa na Uganda mabao 3 kwa 0 mwishoni mwa juma lililopita katika michuano ya kufuzu katika fainali za CHAN zitazofanyika nchini Rwanda mwakani.

Malinzi amesema kuwa Mkwasa atasaidiwa na Kocha wa timu ya taifa ya Zanzibar Hemed Suleiman 'Morocco' hadi mwezi Septemba.

Akizungumza kwa hisia, Kiongpzi huyo wa TFF amesisitiza kuwa anafanya bidii kusaidia kuimarisha soka nchini Tanzania.

Mart Nooij anayeondoka Tanzania amesema licha ya kufutwa kazi, amesema amesaidia kuinua kiwango cha Taifa Stars na anajivunia mfumo wa kuwapa vijana nafasi katika timu ya taifa.

Ameongeza kuwa, “Mwanaweza kunikosoa kwa matokeo mabaya, hiyo ni kawaida katika mchezo wa soka na ndivyo maisha yanavyokwenda na nakubali kwa heshima kubwa lakini kuna ulazima wa kuwapa nafasi vijana chipukizi nafasi kote barani Afrika ili wafikie katika medani ya Kimataifa, hilo ni muhimu sana”.

Nooij kabla ya kujiunga na Tanzania aliwahi kufunza soka katika klabu ya St George ya Ethiopia, Msumbiji na Burkina Faso.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.