Pata taarifa kuu
CECAFA-SOKA

Michuano ya CECAFA yaendelea Dar es Salaam

Siku ya Jumatatu, ni siku ya mapumziko katika michuano ya kuwania ubingwa wa soka baina ya vlabu kutoka eneo la Afrika Mashariki na kati CECAFA kabla ya kuanza kwa michuano ya robo fainali siku ya Jumanne.

Kutoka kushoto, katibu mkuu wa CECAFA, Nicholas Musonye, wa pili kutoka kushoto, Leodegar Tenga, rais CECAFA na Jamal Malinzi, rais wa TFF
Kutoka kushoto, katibu mkuu wa CECAFA, Nicholas Musonye, wa pili kutoka kushoto, Leodegar Tenga, rais CECAFA na Jamal Malinzi, rais wa TFF RFIKiswahili
Matangazo ya kibiashara

Michuano hii inaendelea katika uwanja wa taifa jijini Dar es salaam nchini Tanzania na tayari vlabu vinane vilivyofuzu katika michuano ya mwondoano vimefahamika.

Vlabu hivyo ni pamoja na APR kutoka Rwanda, Gor Mahia ya Kenya, Al Shandy ya Sudan , Yanga na Azam kutoka Tanzania, KCCA ya Uganda, Malakia ya Sudan Kusini na Al Khartoum ya Sudan.

Siku ya Jumanne, APR ambayo iliongoza kundi B kwa alama 9 itachuana katika mchuano wa kwanza na Al Khartoum ya Sudan iliyomaliza ya tatu katika kundi A kwa alama 7.

Mchuano mwingine utakuwa ni kati ya Gor Mahia ya Kenya waliomaliza wa kwanza katika kundi lao kwa alama 10 baada ya kushinda mechi tatu na kwenda sare mchuano mmoja dhidi ya Malakia ya Sudan Kusini iliyofuzu kutoka kundi C.

Siku ya Jumatano, Al Shandy washinda wa pili wa kundi B watachuana na KCCA ya Uganda waliomaliza wa pili katika kundi C kwa alama 6.

Mchuano unaosubiriwa kwa hamu kubwa na mashabiki wa soka nchini Tanzania ni kati ya Azam na Yanga, mchuano ambao kwa mashabiki wa timu hizi mbili umekuja mapema na ni kama fainali ya mwaka 2013.

Fainali ya michuano hii ya CECAFA itachezwa siku ya Jumapili.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.