Pata taarifa kuu
BURUNDI-DRC-SOKA

Intamba mu Rugamba yaangukia pua nyumbani

Timu ya taifa ya Burundi ikichezea nyumbani na timu ya taifa ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (Leopards), imekubali kichapo cha mabao 3-2. Mechi ya marudiano itachezwa hivi karibuni mjini Kinshasa.

Kikosi cha timu ya taifa ya Burundi Intamba mu Rugamba.
Kikosi cha timu ya taifa ya Burundi Intamba mu Rugamba. RFI-KISWAHILI
Matangazo ya kibiashara

Timu ya taifa ya Burundi (Intamba mu Rugamba) imeonyesha mchezo mzuri katika kipindi ha kwanza licha ya kuburuzwa kwa mabao 3-2.

Timu ya taifa ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (Leopards) ndio ilianza kuliona lango la Intamba mu Rugamba katika dakika za mwanzo, bao ambalo liliwekwa kimyani na mchezaji maarufu Yannick Bolasie katika dakika za mwanzo katika kipindi cha kwanza.

Winga wa DR Congo Yannick Bolasie.
Winga wa DR Congo Yannick Bolasie. AFP PHOTO / ISSOUF SANOGO

Intamba mu Rugamba ilikuja juu na kusawazisha dakika chache baadae. Hadi mwisho wa kipindi cha kwanza cha mchezo, timu hizi mbili zilikua sare ya bao moja kwa moja. Hata hivyo katika kipindi cha kwanza cha mchezo, Intamba mu Rugamba ilionekana ikitamba uwanjani na kutawala mpira kwa muda mrefu.

Katika kipindi cha pili, baada ya kocha wa timu ya taifa ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Jean-Florent Ikwange Ibengé kufanya mabadiliko ya wachezaji wawili, Leopards walikuja juu na kulisakama lango la Intamba mu Rugamba. Wakati huo huo Intamba mu rugamba ilipata nafasi nzuri na kufunga bao la pili katika dakika ya 82 ya mchezo. Dadikia nne baadae Leopards walilisakama lango la Intamba mu Rugamba na kusawazisha bao la pili. Bila kuchelewa Leopards waliingiza bao la tatu. Mchezo umemalizika, timu ya taifa ya Burundi ikijikuta imeangukia pua ikiwa nyumbani kwa kufungwa mabao 3-2.

Mechi ya marudiano inatazamiwa kuchezwa hivi karibuni katika mji wa Kinshasa.

Wakati huo huo timu ya taifa ya Togo imefungwa bao 1-0 jijini Lome dhidi ya Uganda katika mzunguko wa pili wamechi ya awali ya kufuzu Kombe la Dunia 2018.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.