Pata taarifa kuu
HISPANIA-SOKA

Luis Enrique ateuliwa kuwa Kocha wa Hispania

Luis Enrique ameteuliwa kuwa Kocha mpya wa timu ya Taifa ya Hispania siku chache baada ya timu hiyo kuondolewa katika fainali za Kombe la dunia.

Kocha mpya wa Timu ya Taifa ya Hispania Luis Enrique
Kocha mpya wa Timu ya Taifa ya Hispania Luis Enrique Wikipedia
Matangazo ya kibiashara

Anachukua mikoba ya Fernando Hierro ambaye alikiongoza kikosi cha Hispania kwa siku 25.

Rais wa Shirikisho la Soka nchini Hispania Luis Rubiales amemtangaza Enrique mwenye umri wa miaka 48, mbele ya vyombo vya habari na kusema anakidhi vigezo vyote vya kupewa nafasi hiyo.

Enrique amewahi kuzifundisha klabu za AS Roma, Celta Vigo na Barcelona ambayo aliifu disha kwa miaka mitatu na kushinda mataji mawili ya Ligi Kuu ya Hispania, mataji matatu ya Copa De Rey na taji ya Ligi ya mabingwa Ulaya mwaka 2005.

Enzi zake akiwa mchezaji Enrique alizitumikia klabu za FC Barcelona na Real Mdrid.

Mapema leo, Shirikisho la soka nchini humo lilimtangaza golikipa wa zamani wa Atletico Madrid na Deportivo La Coruna Jose Francisco Molina kuwa mkurugenzi wa ufundi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.